Christopher Philemon - Uchukuzi
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta Uchukuzi na Mawasiliano), Mhandisi Atashasta Nditiye, amesema ujenzi wa jengo la tatu la abiria wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), kinatarajia kukamilika mwanzoni mwa Agosti mwaka huu kwa kuanza kuhudumia abiria.
Amesema amefurahishwa kwa kukamilika kwa ujenzi wa kiwanja hicho ambapo kwa vimefungwa vifaa vya kisasa.
Akizungumza mara baada ya ziara ya kukagua kiwanja hilo, amesema kuwa katika idadi ya miruko ya ndege Barani Afrika inachukua nafasi ya tano na nafasi ya sita kwa abiria.
‘’ Nimefurahishwa kwa kukamilika kwa ujenzi wa jengo la tatu la abiria wa kiwanja cha Ndege ambapo utakapoanza kuhudumia abiria natarajia tutachukua nafasi mzuri zaidi Barani Afrika kwani ni kiwanja cha kisasa nahuduma zetu ni mzuri,’’ alisema.
Nae Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere( JNIA), Paul Rwegasha, amesema kukamilika kwa jengo hilo litaweza kuhudumia jumla abiria milioni nane kwa mwaka.
Rwegesha alisema ujenzi wa jengo la kwanza lina uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 kwa mwaka na ujenzi wa pili abiria milioni 1.5
Alisema kukamilika kwa Jengo la tatu la abiria litaongeza idadi ya ndege, abiria pamoja na watalii baada ya kuwa na miundombinu bora na yakisasa.
Vile vile alisema ujenzi wa kiwanja cha tatu ni kwa ajili ya abiria wa safari za Kimataifa ambapo kwa sasa yako mashirika na Kampuni 20 na kiwanja cha pili kwa ajili ya abiria wa safari za ndani ya nchi na Kimataifa ambapo yana Kampuni sita huku kiwanja cha kwanza safari za ujumla za ndani ya nchi Kampuni ni 12.
Alisema ujenzi wa jengo la tatu la abiria litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 2,800, kwa saa na maegesho ya magari mchanganyiko yasiopungua 2,075 kwa wakati mmoja.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini(TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama, alisema wako katika maandalizi ya wakuu wanchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa 39 wa SADAC ambapo maadalizi yameambatana na ukarabati wa maboresho ya miundombinu na samani katiaka jengo la pili la Abiria.