Meneja Mawasiliano wa asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Bi. Agnes Kabigi (52)amefariki dunia leo mchana Ijumaa Julai 26,2019.
Agnes Kabigi ambaye ni mwandishi Mwandamizi aliyewahi kufanya kazi katika Magazeti ya Uhuru,Mzalendo na Nipashe amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla wakati akitekeleza majukumu yake wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Taarifa za kifo cha Agnes Kabigi zimethibitishwa na Mkurugenzi wa Shirika la AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa.
"Ni kweli ndugu yetu Agnes Kabigi ametutoka,amefariki dunia huko Kahama baada ya kuanguka akiwa kwenye majukumu ya kikazi" - Dkt. Mwakyusa.
Agnes alizaliwa tarehe 13.7.1967.
ZITTO KABWE AMLILIA AGNES KABIGI
Soma Pia : MWILI WA AGNES KABIGI WAAGWA KAHAMA...WASAFIRISHWA DAR KWA AJILI YA MAZISHI
ZITTO KABWE AMLILIA AGNES KABIGI
Soma Pia : MWILI WA AGNES KABIGI WAAGWA KAHAMA...WASAFIRISHWA DAR KWA AJILI YA MAZISHI
R.I.P AGNES KABIGI
Social Plugin