Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : MWILI WA AGNES KABIGI WAAGWA KAHAMA...WASAFIRISHWA DAR KWA AJILI YA MAZISHI


Mwili wa Meneja Mawasiliano wa asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Bi. Agnes Kabigi umeagwa leo Jumamosi Julai 27,2019 Mjini Kahama mkoani Shinyanga na kusafirishwa kwenda jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazishi.


Agnes Kabigi alifariki dunia jana mchana Ijumaa Julai 26,2019 baada kuanguka ghafla wakati akitekeleza majukumu yake akiwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Agnes Kabigi ni mwandishi Mwandamizi aliyewahi kufanya kazi katika Magazeti ya Uhuru,Mzalendo na Nipashe na mpaka umauti unamkuta alikuwa anafanya kazi katika shirika la AGPAHI linalojihusisha na mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI ambalo linafanya kazi zake katika mikoa ya Shinyanga,Mwanza,Simiyu na Mara.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa shirika la AGPAHI,wakati wa kuaga mwili wa marehemu,Mfanyakazi wa AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Kasablankhahr Herman amesema mwili wa Agnes utasafirishwa kwa ndege majira ya saa 10 leo jioni kutoka Mwanza hadi Jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazishi.

Agnes alizaliwa tarehe Julai 13,1967.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Agnes Kabigi . Amina


Agnes Kabigi enzi za uhai wake

Mwili wa marehemu Agnes Kabigi ukitolewa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama leo Julai 27,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mfanyakazi wa AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Kasablankhahr Herman akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu Agnes Kabigi.
Mfanyakazi wa AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Kasablankhahr Herman akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu Agnes Kabigi.
Mfanyakazi wa AGPAHI akiongoza maombi wakati wa kuaga mwili wa Agnes Kabigi
Kaka wa marehemu akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu Agnes Kabigi.
Zoezi la kuaga mwili wa marehemu likiendelea.
Gari lililobeba mwili wa Agnes Kabigi kuelekea Mwanza kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Dar es salaam

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

ZITTO KABWE AMLILIA AGNES KABIGI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com