Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA TIGO TANZANIA NA TECNO WAZINDUA SIMU MPYA



Meneja wa Bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga, (kushoto) akionyesha kwa waandishi wa habari simu mpya za Smartphone aina ya TECNO S3 na TECNO R7, wakati wa uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Saba Saba jijini Dar es Salaam. (kulia) ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya.
Meneja wa Bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga, (kushoto) akimsikiliza Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya (kulia) wakati akionyesha kwa waandishi wa habari simu mpya za Smartphone aina ya TECNO S3 na TECNO R7, wakati wa uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Saba Saba jijini Dar es Salaam leo
Meneja wa Bidhaa za intaneti wa Tigo,Mkumbo Myonga, (kushoto) akimkabidhi zawadi ya simu aina ya TECNO S3 mmoja wa waandishi wa habari waliojishindia zawadi ya simu wakati wa uzinduzi simu hizo uliofanyika katika viwanja vya Saba Saba.jijini Dar es Salaam (kulia) ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya.
Meneja wa Bidhaa za interneti wa Tigo, Mkumbo Myonga, (kushoto) akiwa na waandishi wa habari waliojishindia zawadi ya simu za TECNO s3 na TECNO S7 wakati wa uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Saba Saba. (kulia) ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya.


*Kuwezesha mteja kupata Intaneti bure kwa mwaka mmoja

Kampuni inayoongoza kwa ubunifu wa kidigitali ya Tigo kwa kushirikiana na kampuni ya kimataifa ya kutengeneza simu za kisasa ya TECNO Mobile ,zimezindua aina mbili mpya ya simu janja za kisasa (smartphones) aina ya TECNO S3 na TECNO R7, katika soko la Tanzania,ambazo zitapatikana kwa bei nafuu na kuwawezesha wateja kufurahia matumizi ya Intaneti kupitia aina za vifurushi watavyochagua kujiunga nayo.

Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika leo katika uwanja wa maonyesho ya Saba Saba,Meneja wa Bidhaa za Intaneti wa Tigo Tanzania,Mkumbo Myonga,alisema kuzinduliwa kwa simu mpya kwa ushirikiano na kampuni ya TECNO Mobile, kwa mara nyingine kunadhihirisha mkakati wa kampuni ya Tigo katika ubunifu wa kidigitali nchini na kufanikisha kuongeza watumiaji wa simu janja,watumiaji wa huduma za data na interneti ya kisasa ya 4G.

“Tunayo furaha kushirikiana na TECNO Mobile leo kuzingua aina mbili za simu janja za kisasa kwa mwaka huu wa 2019.Simu aina ya TECNO S3 na TECNO R7 ni simu zinazatikana katika mtandao wa Tigo pekee katika soko na zinapatikana kwa gharama nafuu ambazo wateja wengi wanamudu kuzinunua”,alisema Myonga.

Myonga alieleza kuwa Tigo inatoa MWAKA MMOJA WA BURE wa kutumia internet kwa wateja watakaozinunua ambapo watakaonunua simu aina ya TECNO R7 watapata (GB54) ambazo zinawezesha matumizi ya internet ya 4G na inauzwa kwa bei ya shilingi 124,900/-.

Kwa wateja watakaonunua simu aina ya TECNO S3,ambayo inawezesha matumizi ya internet ya 3G,watakuwa na uhuru wa kuchagua ofa wanayotaka, ya kwanza MWAKA MMOJA WA BURE wa kutumia internet kutokana na kupatiwa GB 48 na gharama ya kununua simu iyo ni shilingi 95,000/-.Ofa ya pili kwa kunua simu inayouzwa shilingi shilingi 74,900/- na kujipatia internet yenye GB3 ambayo inawezesha mteja kuitumia miezi mitatu bure.Simu hizi mpya katika soko la Tanzania zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini na zitapatikana katika banda la maonyesho la Tigo lililopo katika uwanja wa maonyesho ya Saba Saba.

Kwa upande wake,Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya, alisema kuzinduliwa kwa simu aina ya TECNO S3 na TECNO R7 kupitia mtandao wa Tigo umelenga kuwezesha wananchi wengi kutumia simu janja na kuweza kufurahia mapinduzi ya ubunifu wa kidigitali ya matumizi ya simu hizi.

“Simu aina ya TECNO R7 imetangenezwa ikiwa na kioo cha ukubwa wa inchi 5,ina scanner ya kisasa,kamera yenye uwezo wa mega 5 upande wa mbele na nyuma na flashi inayowezesha kuchua picha kwa kiwango cha ubora wa juu,imetengenezwa kwa ubunifu wa tekbolojia mbalimbali za kisasa zinazowezesha matmizi ya internet na kupiga picha.Simu ya aina ya TECNO S3 imetengenezwa kwa teknolojia za kisasa zinazowezesha matumizi ya teknolojia ya Android Go OS ,inao ukubwa wa kioo cha mbele cha inchi 4,inawezesha matumizi ya teknolojia za GPS na dual SIM,ambazo zimeongezwa katika simu za Tecno tolea la sasa hivi,”alisema Mkomoya.

Simu zote za TECNO S3 na TECNO R7 zina waranti ya miezi 13.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com