Na. Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Wafanyabiashara wa Nyama jijini Dodoma wamesema kuwa katazo la utumiaji magogo katika ukataji wa nyama Ifikapo Septemba 30,2019 katika bucha itakuwa ni changamoto kubwa kwao.
Baadhi ya wafanyabiashara Wanyama katika soko kuu la Majengo Mkoani Dodoma wamesema utumiaji wa Magogo katika ukataji wa nyama walishaizoea enzi na enzi hivyo katazo la Magogo ya kukatia nyama buchani itakuwa changamoto kunbwa kwao.
Anna Francis na Juma Abbas ni miongoni mwa wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya nyama katika soko kuu la Majengo ambapo wamesema katika utumiaji wa Mashine za kukatia nyama patakuwepo na changamoto hususan umeme unapokatika huku changamoto zingine ni chembechembe ya vyuma.
Changamoto nyingine ambazo wamezitaja ni gharama ya kumudu hizo mashine kwa urahisi wa kupatikanaji kwani mara nyingi hupatikana nje ya nchi hususan nchi jirani ya Kenya.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Bodi ya Nyama Tanzania ilisema kuwa ifikapo Septemba 30, 2019 itakuwa mwisho kwa wauza nyama buchani kutumia magogo na endapo mtu atabainika akitumia , hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ambapo Ofisa Usajili kutoka katika bodi hiyo, Geofrey Sosthenes alibainisha kuwa magogo yanasababisha hasara ya upotevu wa nyama, kitaalamu katika kilo 100 inapotea kilo moja, ambapo kwa mwaka muuzaji hupoteza Sh. milioni 3.8 ambayo inatosha kununua machine ya kisasa ya kukatia nyama.
Social Plugin