Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo (SMT) Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu (SMZ) Bi Mansura Mosi Kassim wameongoza kikao cha mashirikiano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania katika sekta ya Kilimo.
Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya ofisi ya Makamu wa Rais Muungano kwa wizara zote za SMT na SMZ kukutana na kuzungumzia Mashirikiano baina yao.
Vikao kama hivyo hutuama kujadili kwa pamoja namna ya kutatua changamoto za Muungano zilizopo katika sekta ya Kilimo.
Katika kikao hicho kumejadiliwa kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali yaliyowekwa katika kikao cha makatibu wakuu wa sekta ya Kilimo kilichofanyika mwezi Machi, 2018.
Kadhalika, maeneo mengine ya mashirikiano yaliyojadiliwa ni pamoja na Maendeleo ya mazao, utafiti na mafunzo, huduma za umwagiliaji na Zana za Kilimo na Sera, na Mipango na uimarishaji wa takwimu.
Kikao kazi hicho kilifanyika tarehe 24 Juni, 2019 katika ofisi za wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar.
Social Plugin