Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao
Kijana aliyejulikana kwa jina laHassan Tungu (26) amefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi wakati akichimba kifusi kwa ajili ya matumizi ya kujengea nyumba katika Kitongoji cha Ngaka, Kijiji cha Nyambui, Kata ya Tinde Wilaya ya Shinyanga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea jana Ijumaa Julai 26,2019 majira ya saa tano na dakika 40 asubuhi.
"Hassan Tungu aliangukiwa na kifusi wakati akichimba kifusi kwa ajili ya matumizi ya kujengea kisha kufa papo hapo. Baada ya kifusi hicho kuanguka pia kiliwajeruhi watu wawili ambao ni Mihambo Mjiga (20) na Elias Magwala (26) wote wakazi wa Tinde na wanapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Tinde",amesema Kamanda Abwao.
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin