Waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Kata ya Sepuka.
Marehemu Elizabeth Said enzi za uhai wake.
Viongozi wa dini kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Sepuka wakielekea eneo ilipofanyika ibada ya kuaga mwili wa marehemu.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Elizabeth Said.
Mkwe wa marehemu, Joseph Helman akisoma historia ya marehemu.
Diwani wa Kata ya Sepuka Yusuf Misanga akizungumza
Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu akitoa pole kwa wafiwa.
Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu akimfariji mme wa marehemu Mzee Andrew Lissu.
Ibada ikiendelea
Wananchi wakiwa kwenye msiba huo
Mme wa marehemu Mzee Andrew Lissu, akimuaga kipenzi mke wake.
Mwili wa marehemu ukiagwa
Hapa ni vilio tu na huzuni.
Na Dotto Mwaibale, Sepuka Singida
MBUNGE wa Singida Magharibi Elibariki Kingu ameongoza mamia ya wananchi katika mazishi ya mke wa Diwani mstaafu wa Kata ya Sepuka Andrew Lissu yaliyofanyika leo kwenye makaburi ya kata hiyo.
Mazishi hayo yaliongozwa na Wachungaji kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Sepuka na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wadini zote za Kiislam na Wakristo.
Akizungumza katika mazishi hayo Kingu aliwapa pole wanafamilia hao kwa kuondokewa na mpendwa wao ambaye alikuwa kipenzi cha watu katika Kata hiyo na maeneo mengine ya jirani.
Katika mazishi hayo viongozi mbalimbali walipata fursa ya kuzungumza na kumtaja marehemu Elizabeth Said aliyefariki juzi kuwa alikuwa ni mama wa mfano katika jamii ya kata hiyo.
Kwa upande wa viongozi wa dini walisisitiza kudumisha amani ya nchi na kujiandaa kiroho kwa kumcha mwenyezi mungu kwani hakuna mtu anayejua ni lini atakufa.
Social Plugin