Korea Kaskazini imefyatua tena makombora mawili ya masafa mafupi leo, ikieleza kuwa ni onyo kwa Korea Kusini dhidi ya mpango wake wa kufanya mazoezi ya kijeshi pamoja na Marekani.
Korea Kusini imesema, makomobora hayo mawili yalirushwa kutoka eneo la Winsan la pwani ya mashariki majira ya alfajiri, na kuruka umbali wa kilomita 250 hadi baharini.
Korea Kaskazini imepigwa marufuku kurusha kombora chini ya maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lakini hii ni mara ya pili kufanya hivyo katika kipindi cha wiki moja, licha ya mkutano kati ya kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un na Rais wa Marekani, Donald Trump mwezi uliopita.
Marekani na Korea Kaskazini wamekuwa wakishiriki katika mchakato wa kidiplomasia wa muda mrefu, kuhusu mpango wa makombora wa Korea ambao umepelekea viongozi wa mataifa hayo mawili kukutana mara tatu tofauti katika mwaka mmoja.