Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano nchini (TCRA) kutoa taarifa za waliohusika kudukua mawasiliano ya simu ya mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na watu wengine.
Wiki iliyopita sauti fupi za mazungumzo ya simu yanayomhusisha Nape, aliyekuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba na makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii
Akizungumza na vyombo vya habari jana Julai 22, Kubenea alisema kitendo kilichofanyika ni kinyume cha katiba na sheria za nchi ambazo zinatoa uhuru wa faragha kwa mtu.
“Hii ni hatari sana kama viongozi wanafanywa hivi kwa mambo ya faragha kutolewa si hata baadaye watu wanaweza kuvunja ndoa za watu, kama Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amezungumza na hawara kwa mfano ikatoka nje si jambo la hatari hili, kuna vitu ambavyo vinatakiwa kuwa na usiri kwa maana kama hawa ni viongozi tu je wananchi wa kawaida inakuaje..?
"Haya mambo hayawezi kufanyika katika nchi inayojali utu wa mtu. TCRA itoe taarifa, ni nani aliyefanya kazi hiyo chafu." Alisema
Social Plugin