Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo Julai 17 amezindua soko la Kimataifa la Madini na Vito Dar es salaam ikiwa utekelezaji wa agizo alilotoa Rais Dkt. John Magufuli kwa kutaka kila mkoa kuwa na soko hilo.
Makonda amesema uwepo wa soko hilo litasaidia wananchi kununua Madini na vito halali na kupunguza matapeli waliokuwa wakiuzia wananchi na Wageni madini na vito feki.
Aidha Makonda amesema uzinduzi wa soko hilo umekuja wakati muafaka ambao Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa wakuu wa nchi za SADC ambao wataingia nchini mwezi ujao wakiambatana na wafanyabiashara amapo pia anaamini watapata nafasi ya kutembelea soko hilo.
Hata hivyo Makonda amesema ndani ya soko hilo yanapatikana madini ya aina zote hivyo amewataka wananchi kulitumi kwakuwa ni halali na linatambulika na serikali.
Itakumbukwa kuwa mkoa wa Dar es salaam ndiyo Soko na lango kuu la Madini hivyo uwepo wa soko hili ni fursa kwa wachimbaji, wafanyabiashara na wananchi kupata madini na vito halali kwa bei halali.
Social Plugin