Mali za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), zinatarajiwa kupigwa mnada Julai 6, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneers & General Traders ya jijini Dar es Salaam, mali zitakazopigwa mnada ni kila kitu kilichokuwamo ndani ya Ukumbi wa Bilicanas uliopo Mtaa wa Mkwepu, jijini Dar es Salaam.
“Mnada huo utafanyika kuanzia saa nne asubuhi kwenye ghala la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) karibu na geti namba 3, bandarini,” imesema taarifa hiyo.
Social Plugin