Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAKA AUA DADA YAKE BAADA YA KUMKUTA KALALA NA JAMAA KAHAMA

Binti aitwaye Suzana Bundala (21) mkazi wa kijiji cha Bugoshi kata ya Uyogo wilayani Kahama ameuawa kwa kupigwa na kaka yake Daudi Bundala baada ya kumkuta live dada yake huyo  akiwa amelala na mpenzi wake Eddy Nkimbila kama mme na mke ndani ya nyumba yao.


Kwa Mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Julai 12,2019 majira ya saa tano usiku ambapo Daudi Bundala alimuua dada yake kwa kumpiga na kitu kizito kichwani.

"Chanzo cha tukio hilo ni marehemu kukutwa akiwa amelala na mpenzi wake aitwaye na Eddy Nkimbila nyumbani kwao kitendo ambacho kilimchukiza mtuhumiwa",ameeleza Kamanda Abwao.

Amesema mtuhumiwa wa mauaji hayo alikimbia baada ya tukio hilo na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea na kwamba mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa taratibu za mazishi. 

"Natoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuacha kujichukulia sheria mkononi na kufikia kufanya matukio ya kikatili kama hili, kwani sheria zitachukua mkondo wake",amesema .
 Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com