UONGOZI wa Azam FC umepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha shabiki wa timu hiyo, Annely Mdendeni, kilichotokea kwa ajali ya gari eneo la Msata, Pwani usiku wa kuamkia leo Jumamosi Julai 27,2019.
"Azam FC tunamkumbuka Mdendeni kama mmoja wa mashabiki waliojitolea kwa vitendo katika kuisapoti timu hiyo katika mechi zake mbalimbali akiwa sehemu ya kundi maarufu la mashabiki la 'Azam Die Hard Fans'.
Aidha uongozi wa Azam FC, unatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki walioguswa na msiba huo na kuwaombea afya njema majeruhi wote waliokuwemo kwenye ajali hiyo warejee katika hali yao ya kawaida".
Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina
Innah Lillahi wainna ilaihi Rajiuun! #RIPAnnely
Social Plugin