MFUKO WA HIFADHI YA JAMII KWA WATUMISHI WA UMMA [PSSSF] WATUMIA BILIONI 122 KULIPA KIINUA MGONGO KWA WASTAAFU

Na.Faustine  Gimu Galafoni,Dodoma.

Mfuko wa  Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma[PSSSF] kuanzia Juni 1 hadi Julai 24,2019   umelipa kiinua mgongo kwa wastaafu  elfu  mbili ,mia sita na hamsini[2,650] huku zikitumika Tsh.Bilioni 122.9  kulipa wastaafu hao.

Hayo yamesemwa Julai 24,2019 jijini Dodoma na Meneja kiongozi ,uhusiano wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii  kwa Watumishi wa Umma[PSSSF] Bi.Yunis Chiume wakati akitoa taarifa ya Maendeleo ya Mfuko huo kwa  vyombo vya habari.

Bi.Chiume amesema kuwa ,PSSSF  unaendelea na jukukumu lamsingi la   kulipa pensheni kwa wastaafu ambapo pia umelipa  pensheni ya Mwezi kwa wastaafu laki moja,ishirini na sita elfu na arobaini na tatu[126,043]  na kiasi kilichotumika ni  Tsh.Bilioni 92.7.

Aidha,Bi.Chiume amesema idadi ya wastaafu ambao  hawajalipwa mafao imepungua kutoka wastaafu 227  Mwezi Mei,2019 na kubaki wastaafu 119 hadi sasa na sababu zinazosababishwa kutolipwa kwa wastaafu hao ni pamoja na kukosa kwa viambatanisho ,pingamizi la waajiri juu ya vyeti feki,kupokea mshahara baada ya kustaafu,na kutofautiana kwa sababu ya kustaafu kati ya nyaraka halisi na mfumo wa utumishi huku juhudi zikiendelea kufanyika  ili kutatua mapungufu hayo    ili wanachama  waweze  kupata mafao  kwa mujibu wa sheria.

Bi.Chiume ameongeza kuwa baada ya mifuko ya PPF ,LAPF,GEPF,na PSPF kuunganishwa na kuundwa PSSSF tarehe 1,Agost,2019 serikali inafanya tathmini juu ya Mafao ya Uzazi  na tathmini hiyo ikikamilika taarifa itatolewa kwa umma .

Kuhusu mfumo wa  Malipo wa Government Electronic Payment Gatway[GePG]  Bi.Chiume amesema umeleta faida kwa mwajiri kujifanyia tathmini ya michango inayotolewa na PSSSF ,Kujitengenezea Ankara za malipo  ,kutengeneza control number,kuweka hesabu sawa,kuweza kupata risiti kwa wakati,kupunguza safari za kwenda kwenye ofisi za mfuko.

Na Faida kwa Mfuko ni kuongeza uwazi,ufanisi,kukusanya michango kwa wakati,mawasiliano rahisi na kutambua wanaowasilisha michango kwa wakati.

Pia ,Bi.Chiume amegusia juu ya suala la mfumo wa Majalada ya kielektroniki [Paperless  Work  Envinronment ]ambapo mfuko wa PSSSF Umeanza kutumia mfumo huo kwa kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali  na kuongeza ufanisi na kupunguza matumizi ya karatasi.

Sanjari na hayo ,katika kueneza elimu kwa umma,PSSSF imeshiriki katika maonesho 43 ya kimataifa ya  Dar Es Salaam na Jumla ya Wastaafu 381 na wanachama na wananchi wengine 1,040  walihudumiwa  huku mfuko huo wa PSSSF Ukitarajia kushiriki kutoa huduma na Elimu kwa wananchi kwenye maonyesho ya Wakulima Nanenane Agosti 1 hadi 8 ,2019 yatakayofanyika katika eneo la Nyakabindi ,Bariadi ,Simiyu  huku maonesho mengine ya PSSSF  yakitarajia kufanyika katika mikoa ya Ruvuma,Mbeya na Morogoro.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post