Mke wa mtawala wa Dubai Sheikh Mohammed Al Maktoum, Binti Mfalme Haya Bint al-Hussein, yuko mafichoni jijini London akidaiwa kuhofia usalama wa maisha yake baada ya kumtoroka Mumewe.
Sheikh Mohammed mwenye miaka 69, ambaye ni Bilionea, aliandika utenzi wenye hisia za hasira kwenye ukurasa wa Instagram akimshutumu mwanamke ambaye hakufahamika kwa vitendo vya ”udanganyifu na usaliti”.
Mke wa kiongozi huyo mzaliwa wa Jordan ana miaka 45, aliolewa na Sheikh Mohammed mwaka 2004 na kuwa mke wa sita, ”mke mdogo”.
Sheikh Mohammed ameripotiwa kuwa na watoto 23 kutoka kwa wake zake.
Binti mfalme Haya awali alitorokea Ujerumani mwaka huu kutafuta hifadhi. Hivi sasa anaelezwa kuishi kwenye nyumba ya thamani ya pauni milioni 85 Kensington Palace Gardens, katikati mwa jiji la London, akijiandaa kufungua mashtaka kwenye mahakama ya juu.
Social Plugin