Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWAKYEMBE:UNGANISHENI NGUVU KATIKA KUENEZA LUGHA YA KISWAHILI

Na.Faustine Gimu  Galafoni,Dodoma.

Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dokta Harrison  Mwakyembe   ameziagiza idara za kisekta   kwa  Pande zote  mbili za Muungano kuunganisha nguvu  katika kueneza Lugha ya Kiswahili kwa Mataifa Mbalimbali.

Dokta Mwakyembe amesema hayo jana Julai 2,2019  jijini   Dodoma katika kikao cha   Ushirikiano baina ya Wizara  ya Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo pamoja na Serikali ya Mapinduzi ,Zanzibar hususan katika masuala ya sanaa,Utamaduni ,na Habari.

Waziri Mwakyembe amesema lengo la kikao hicho ni kujadili Masuala ya Muungano katika sekta ya Habari na kubadilishana Ushirikiano na uzoefu  ambapo pia wamepokea taarifa ya Makatibu wakuu   juu ya Ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivyo,Dokta Mwakyembe amesema  mahitaji ya Lugha ya Kiswahili katika mataifa mbalimbali ya ulimwengu ni mkubwa ni wakati sasa serikali  zote za Muungano zikajipambanua vyema katika ushirikiano wa kueneza lugha hiyo.

Katika hatua nyingine Dokta Mwakyembe  ameyaagiza shirika la  Umma la Utangazaji Tanzania [TBC] na Shirika la Umma la Utangazaji  Zanzibar,[ZBC] Kuwa na ushirikiano wa Pamoja katika Uzalishaji wa Vipindi vya  runinga  ya Taifa ya Utalii,Safari Channel ili kutangaza utamaduni ,mali kale na vivutio vilivyopo    Tanzania  kwa ustadi mkubwa hali itakayosaidia  kukuza utalii hapa nchini.

Pia katika maafikiano ya mkutano huo Waziri Mwakyembe amesema pande zote mbili za muungano zitashiriki katika maandalizi ya tamasha kubwa la utamaduni Afrika  Mashariki  litakalofanyika Mwezi Septemba Jijini Dar Es Salaam  huku mapendekezo mengine ya mkutano huo ni idara zote za kisekta   kushiriki pamoja katika maandalizi ya bajeti kuwezesha timu ya taifa inaposhiriki mashindano mbalimbali ya Kimataifa.

Sekta ambazo zimeshiriki  katika mkutano huo  wenye lengo la kukuza utamaduni,Sanaa ,Habari na Lugha ya Kiswahili ,ni sekta ya utamaduni,Sekta  ya Utalii,Sekta ya Habari na Sekta ya Sanaa na Michezo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com