Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dokta Harrison Mwakyembe ameziagiza idara za kisekta kwa Pande zote mbili za Muungano kuunganisha nguvu katika kueneza Lugha ya Kiswahili kwa Mataifa Mbalimbali.
Dokta Mwakyembe amesema hayo jana Julai 2,2019 jijini Dodoma katika kikao cha Ushirikiano baina ya Wizara ya Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo pamoja na Serikali ya Mapinduzi ,Zanzibar hususan katika masuala ya sanaa,Utamaduni ,na Habari.
Waziri Mwakyembe amesema lengo la kikao hicho ni kujadili Masuala ya Muungano katika sekta ya Habari na kubadilishana Ushirikiano na uzoefu ambapo pia wamepokea taarifa ya Makatibu wakuu juu ya Ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivyo,Dokta Mwakyembe amesema mahitaji ya Lugha ya Kiswahili katika mataifa mbalimbali ya ulimwengu ni mkubwa ni wakati sasa serikali zote za Muungano zikajipambanua vyema katika ushirikiano wa kueneza lugha hiyo.
Katika hatua nyingine Dokta Mwakyembe ameyaagiza shirika la Umma la Utangazaji Tanzania [TBC] na Shirika la Umma la Utangazaji Zanzibar,[ZBC] Kuwa na ushirikiano wa Pamoja katika Uzalishaji wa Vipindi vya runinga ya Taifa ya Utalii,Safari Channel ili kutangaza utamaduni ,mali kale na vivutio vilivyopo Tanzania kwa ustadi mkubwa hali itakayosaidia kukuza utalii hapa nchini.
Pia katika maafikiano ya mkutano huo Waziri Mwakyembe amesema pande zote mbili za muungano zitashiriki katika maandalizi ya tamasha kubwa la utamaduni Afrika Mashariki litakalofanyika Mwezi Septemba Jijini Dar Es Salaam huku mapendekezo mengine ya mkutano huo ni idara zote za kisekta kushiriki pamoja katika maandalizi ya bajeti kuwezesha timu ya taifa inaposhiriki mashindano mbalimbali ya Kimataifa.
Sekta ambazo zimeshiriki katika mkutano huo wenye lengo la kukuza utamaduni,Sanaa ,Habari na Lugha ya Kiswahili ,ni sekta ya utamaduni,Sekta ya Utalii,Sekta ya Habari na Sekta ya Sanaa na Michezo.
Social Plugin