Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika [ CPA] inakusudia kujenga ofisi ya Makao makuu ya Jumuiya hiyo pamoja na ujenzi wa Hotel ya Nyota tano katika eneo la Ndejengwa Jiji la Dodoma.
Hayo yamebainishwa jana Julai 12,2019 na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madola ya Afrika,Muturi Jastine Muturi.
Muturi ambaye pia ni Spika wa Bunge la Nchi ya Kenya amesema amevijunia kutokana na kujionea hatua mbalimbali za awali za upimaji na uwekaji wa Michoro mbalimbali katika eneo hilo ambapo amesema ni eneo kubwa na linatosheleza katika masuala mbalimbali ya Uwekezaji wa Majengo ya Jumuiya hiyo.
Muturi Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya ukaguzi wa Eneo hilo alisema kuwa eneo utawezesha ujenzi wa ofisi za jumuiya ya CPA na ujenzi wa vivutio pamoja na ujenzi wa Hotel ya nyota tano.
"Kwanza napenda kutoa shukrani kwa serikali ya Tanzania kwa kuweza kutoa eneo kwa ujenzi wa Ofisi ya CPA, Tulipewa eneo siku nyingi lakini leo ndo tumekuja kuliona.
"Kabla ya mwaka huu Kuisha tunatarajia kuanza ujenzi wa mradi wetu na pamoja na kuwa hatujafanya tathimini ya kutosha mradi huo unaweza kugharimu kiasi cha cha dola milioni 30"alisema Muturi.
Muturi pamoja na wajumbe wengine wa Jumuiya hiyo wakiongozana na Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugui walifanya ziara nchini Jijini Dodoma kwa lengo la ukaguzi wa ujenzi wa ofisi za Wizara mbalimbali katika mji wa serikali.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema Dodoma ni jiji ambao ni kiunganishi cha Tanzania na Mataifa mengine ya Afrika na Duniani kwa ujumla serikali inaendelea uimarishaji wa Miundombinu mbalimbali kama vile uwanja wa ndege Msalato pamoja na reli.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe alisema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa Jiji la Dodoma unafanya kazi ya kupima Viwanja na kuweka miundombinu ambayo unaweza kumfanya mtu yoyote kuweza kujenga muda wowote.
Katika hitimisho la ziara hiyo ,Spika wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai ameshukuru ujio huo wa Mwenyekiti Wa CPA hapa nchini na kuahidi kuwa wataendeleza ushirikiano .
Ujumbe huo Jumuiya ya Madola ya Mabunge ya Afrika,[CPA] ulitembelea miradi mbalimbali katika jiji La Dodoma kama vile, ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo mikoani, mji wa Serikali mtumba ,Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),Ukumbi wa mikutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja kukagua eneo la Ndejengwa [A PLAN OF NDEJENGWA INVENSTMENT AREA] ambalo jumuiya hiyo itajenga ofisi hizo pamoja na eneo la kitegauchumi kitegauchumi.