Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mhandisi Samuel Mafwenga, amesema kelele zaidi ya viwango, zinasababisha upungufu wa nguvu za kiume pamoja na kuleta athari za akili na afya ya ubongo.
Hayo ameyabainisha leo Julai 24, katika mkutano wa wamiliki wa baa, kumbi za starehe na sherehe na kuzungumzia kuhusu kelele zaidi ya viwango vilivyoainishwa katika kanuni za mwaka 2015 za viwango vya udhibiti wa uchafuzi kelele na mitetemo, ambapo amesema tangu mwaka 2016 hadi 2019, wamepokea malalamiko 4,790 ambapo kati ya hayo 952, sawa na asilimia 20 ni ya kelele.
Amesema tafiti zinaonyesha kelele zina athari kwa Watoto kiakili, kiafya na kwa wajawazito na wazee pia.
"Tatifiti zinaonyesha kelele zina athari ya faragha pia hivyo kusababisha upungufu wa nguvu za kiume hivyo ni vyema kuzingatia viwango vilivyopendekezwa kulingana na maeneo," amesema Mafwenga.
Ameongeza ili kuondoa kero hiyo ndani ya jamii ni vyema wamiliki wakatumia vifaa vya kupunguziwa Kelele ili waweze kupima viwango vyao.
Chanzo - EATV
Social Plugin