Baba wa watoto kumi huko nchini Nigeria, aitwae Malayu Ibrahim, ameunguzwa sehemu zake za siri na mke wake baada ya kumwambia anataka kuongeza mke wa pili.
Baba huyo alikimbizwa hospitali usiku wa Julai 12, 2019, baada ya kurudi nyumbani kwake na kumwagiwa maji ya moto na ameeleza kuwa,
"Nilirudi nyumbani na kumueleza mke wangu nataka kuongeza mke wa pili ambaye tutakuwa pamoja katika maombi na sala, baada ya kumueleza vile alionekana mwenye furaha na tuliishi kwa amani pamoja na sikuona mabadiliko yoyote kwake, lakini kuna siku nilirudi na nyama nyumbani, akaenda kuchemsha kisha alirudi na maji ya moto na kunimwagia sehemu zangu za siri kuanzia mapajani."
Pia Malayu Ibrahim akaongeza kwa kusema yeye kazi yake ni mwalimu wa shule ya msingi, yeye pamoja na mkewe wamebahatika kupata watoto kumi mpaka sasa.
Social Plugin