NA SALVATORY NTANDU
Serikali imesema haitasita kuzivunja Bodi za Usimamizi wa Maji na kuwaondoa katika nyazifa, Wakurugenzi wa Mamkala hizo watakaobainika kushindwa kukusanya mapato na kusababisha kushindwa kujiendesha ikiwa ni pamoja nakukosekana kwa huduma ya maji kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa jana wakati akizungumza na watumishi wa Mamkala ya majisafi na Usafi wa Mazingira mjini kahama(KUWASA) nakusema kuwa,mamlaka za maji hapa nchini nyingi zinashindwa kujiendesha na kusababisha kwa wananchi kukosha huduma hiyo muhimu.
Amesema ofisi yake inahitaji kupata taarifa za ukusanyaji wa mapato(akra) kila baada ya miezi mitatu na nisipoyapata navunja bondi ya maji na kumuondoa mkurugenzi kwenye nafasi yake na kumpatia mwingine mwenye uwezo wa kukusanya mapato na kupeleka huduma ya maji kwa wananchi.
"Nimevunja bodi na kumuondoa mkurugenzi wa mamlaka ya maji Morogoro kutokana na kushindwa kukusanya mapato na kusababisha huduma ya maji kwa wananchi kukosekana, na nitafanya hivyo pia kwenye mamlaka ambazo zitashindwa kukusanya mapato bila kujali mwenyekiti wake wa bodi ni rafiki yangu" Amesema Prof.Mbalawa.
Hata hivyo Prof Mbarawa amesema mamlaka za maji zimekuwa zikisuasua kupeleka huduma ya maji hata kilometa mbili kwa wananchi na badala yake wamekuwa wakiomba fedha wizarani na huku wamekuwa wakitoa huduma na kukusanya mapato na kushindwa kutatua kero za wananchi.
Hata hivyo Prof. Mbarawa amesema adhima ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 asilimia 85 ya vijiji vyote nchini view vinapata maji safi na salama hivyo kuzitaka mamlaka hizo kuongeza mitandao ya maji ili kuongeza mapato na kusogeza huduma hiyo kwa wananchi.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama(KUWASA )Meja mstaafu Bahati Matala amesema, atahakikisha anaongeza mapato kwenye mamlaka yake kwa kupanua mtandao wa maji na kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.
Amefafanua kuwa, fedha itakayopatikana kwenye ukusanyaji wa akra za maji atahakikisha apeleka huduma ya maji kwa wananchi nakuongeza kwa wale wafanyakazi ambao watabainika kuwaunganishia huduma ya maji wateja kinyemela hata sita kuwaondoa kazini.
Social Plugin