Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PUMA ENERGY TANZANIA YAAHIDI KUENDELEA KUTOA ELIMU YA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI NCHINI KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde (wa pili kushoto), akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni nne kwa mshindi wa kwanza wa shindano la michoro ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi mwaka 2019, Alphonce Philipo wa shule ya msingi Jenerali Musuguri, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, waandaaji wa shindano, Dominic Dhanah

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde,akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, waandaaji wa shindano, Dominic Dhanah,akisoma taarifa katika utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, waandaaji wa shindano, Dominic Dhanah,akifurahia jambo na wanafunzi (hawapo pichani) wakati akisoma taarifa inayohusu utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Mratibu wa mafunzo ya Elimu ya usalama barabarani kutoka Amend Bi.Neema Swai,akiongea wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Mwalimu wa shule ya Msingi ya General Musuguri,Beatrice Chidumizi,akitoa pongeza kwa Puma Energy wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Afisa Elimu Msingi jiji la Dodoma,Joseph Mabeyo,akitoa shukrani kwa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde (wa pili kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, waandaaji wa shindano, Dominic Dhanah, wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Mwalimu wa shule ya msingi Kaloleni Bi.Edina Kagulumbega,akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Sehemu ya Wanafunzi kutoka shule za msingi wakifuatilia hafla ya utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Baadhi ya walimu wakifuatilia utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Wanafunzi wakiimba wimbo maalumu wa unaoelezea umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani wakati wa utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Mmoja wa wanafunzi waliopata elimu ya mafunzo ya usalama barabarani akionesha mfano wa mwanafunzi aliyepata ajali kwa kutozingatia sheria za usalama barabarani wakati wa utoaji zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Wakiangalia michoro ya usalama barabarani iliyochorwa na wanafunzi kutoka shule tano za msingi katika jiji la Dodoma kabla ya kumtangaza mshindi wa shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano la michoro ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi mwaka 2019, hafla ambayo imefanyika jijini Dodoma.
......................

*Ni katika mkakati wake wa kukomesha ajali nchini, wanafunzi Dodoma wanufaika
*Naibu Waziri Mavunde awapongeza, asema ni kampuni ya mfano...atoa maombi maalum
Na Said Mwishehe,Michuzi TV -Dodoma
KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania imesema itaendelea kutoa elimu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa shule za msingi mbalimbali nchini ikiwa ni mkakati wake wa kupunguza ajali nchini.
Pamoja na ahadi hiyo kampuni hiyo imetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi zaidi ya 4500 katika shule tano za msingi katika Jiji la Dodoma kwa mwaka huu wa 2019 huku ikiahidi kuendelea kutoa elimu hiyo na kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia wanafunzi wengi zaidi ambao watakuwa mabalozi kwa wengine.
Akizungumza leo Julai 25 jijini Dodoma mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Vijana Athony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah amesema programu hiyo ya mwezi mmoja kwa Dodoma ilihusisha mafunzo ya usalama barabarani kwa walimu 15 na wanafunzi 4500, katika shule tano.
Amefafanua kulikuwa na shindano la uchoraji wa michoro inayo hamsisha usalama barabarani ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni iliyozinduliwa rasmi mwaka 2013 ambapo zaidi ya shule 80 zimefikiwa huku wanafunzi 100,000 wakiwa wamepatiwa mafunzo katika mikoa ya Dar-es-salaam, Geita, Ruvuma na Dodoma.
“Puma Energy Tanzania imeamua kuja jijini Dodoma kwa sababu ya ukuaji wa haraka wa jiji hili ambapo shughuli za kijamii na ongezeko la watu na magari ambayo yanahatarisha usalama wa watoto wanapokwenda shuleni na kurudi nyumbani,",amesema Dhanah na kuongeza “Hadi sasa tumeweza kufundisha wanafunzi zaidi ya 4500 wa shule tano za msingi zilizopo jiji la Dodoma".
Dhahana amesema mafunzo hayo ya usalama barabarani na uchoraji alama za barabarani ni kipaumbele kwa lengo la kuwapa uelewa watoto hususani wa shule za msingi juu ya namna bora ya matumizi ya barabara.
Alibainisha lengo ni kuwafanya watoto kuwa na uelewa wa matumizi ya barabara ili kuongeza uelewa kuhusu dhima nzima ya usalama barabarani kwa Watanzania.
“Lengo letu kama kampuni ni kuongeza wigo ili kufikia shule nyingi zaidi nchi nzima. Puma Energy Tanzania itaendelea kuwekeza katika kampeni ya usalama barabarani ikishirikiana na serikali kupitia jeshi la Polisi ili kuokoa maisha ya watanzania,” amebainisha.
Akieleza zaidi amesema unzo hayo yametolewa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kupitia Shirika lisilo la kiserikali la Amend ambapo elimu hiyo pia imetolewa kwa walimu 15 wa shule hizo.
Awa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Ajira na Vijana Anthony Mavunde amesema Puma Energy Tanzania ni kampuni iliyoamua kutoa elimu ya usalama barabara nchini huku akitoa ombi kwa kampuni hiyo kufundisha walimu hizo ili wakifundisha masomo ya kawaida wawe pia wanataka na elimu ya usalama.
Amesema kwa kufanya hivyo inasaidia kupunguza ama kumaliza kabisa ajali za barabarani huku akifafanua Serikali itaendelea kuweka alama za usalama barabarani ili kuondoa changamoto za ajali.
Amesema kuwa kutokea kwa elimu hiyo kwa Jiji la Dodoma kunakwenda kutengeneza jamii yenye mabalozi wazuri katika kutoa elimu ya usalama barabarani huku akieleza Dodoma ni ya pili kwa mtandao wa barabara za lamo,hivyo ni muhimu elimu hiyo kuendelea kutolewa.
"Nimesikia ombi la walimu na wanafunzi la kuhitaji alama za barabarani, hivyo Serikali itaendelea kuweka alama hizo.Pia nimezungumza na wenzetu wa Puma wamekubali kupaka rangi za usalama barabarani na wataanza na shule tano ambazo zimepatiwa elimu hii ya usalama barabarani,"amesema Mavunde
Wakati huo huo walimu wakuu katika shule za msingi katika Jiji la Dodoma wametoa ombi la kuweka alama za barabarani na hasa alama za pundamilia au matuta ili kuhakikisha wanafunzi wanapovuka wanakuwa salama kwani barabara nyingi hazina alama hizo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi General Musuguri Beatrice Chidumizi amesema changamoto iliyopo kwenye eneo la shule yao ni kukosekana kwa matuta au alama za barabarani, hivyo wanalazimika kumuweka mtu wa kuvusha wanafunzi ambaye analipwa fedha.
"Changamoto kubwa iliyopo katika shule yetu ni barabara yetu kutokuwa na matuta na alama za pundamilia,hivyo tunaomba tuwekewe alama za barabarani kwa ajili ya usalama wa wanafunzi wetu.Tunaishukuru Puma kwani imetusaidia sana kuwajengea uelewa wanafunzi wetu na sasa wanafahamu cha kufanya wanaoutaka kuvuka barabara.
"Tunaamini kupitia mafunzo haya tutapunguza ajali kwa watoto wetu na watumiaji wengine wa barabara zetu,"alisema Mwalimu Chidumizi na kuongeza kuwa umefika wakati kwa elimu hiyo kuendelea kutokea kwa Jiji la Dodoma hasa kwa kuzingatia Dodoma inakuwa kwa kasi kutokana na Serikali kuhamia Dodoma.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com