Rais wa Tunisia, Beji Caid Essebsi amefariki dunia leo Alhamisi Julai 25, katika hospitali ya kijeshi mjini Tunis akiwa na umri wa miaka 92, baada ya kuugua kwa kipindi kirefu.
Taarifa zinasema Essebsi alipelekwa hospitalini hapo jana jioni kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja.
Rais huyo alikuwa kiongozi mkongwe zaidi duniani baada ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza na amekuwa madarakani tangu mwishoni mwa mwaka 2014 baada ya kushinda uchaguzi huru wa kwanza kufuatia vuguvugu la maandamano katika mataifa ya kiarabu.
Mapema mwaka huu, Essebsi alitangaza kwamba hatogombea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa Novemba mwaka huu alisema kwamba muda umewadia kwa kijana kushika nafasi hiyo ya uongozi.
Social Plugin