Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mkuu wa Mkoa Wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge ametoa agizo kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima[TIRA] kwa kanda ya kati Kuhakikisha inafuatilia na kuzichukulia hatua za kisheria kampuni za Bima ambazo zimekuwa zikiharibu utoaji wa huduma kwa wananchi.
Dokta Mahenge ametoa agizo hilo Julai 18,2019 wakati wa ufunguzi siku ya maadhimisho ya Bima kwa kanda ya kati ambayo imeanza Julai 17 hadi 19,2019 yakifanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Dokta Mahenge amebainisha kuwa pamekuwepo na changamoto kwa baadhi ya makampuni ya Bima kushindwa kutoa huduma ipasavyo na kutotoa huduma ya fidia kwa wakati ,kwa wateja na badala yake yamekuwa yakitoa huduma hafifu huku lengo lake ni kunyonya haki zao pindi wanapokumbwa na majanga licha ya kuwa na vigezo vyote hivyo Wakati umefika sasa kwa Mamlaka ya usimamizi wa Bima[TIRA]kuzichukulia hatua kampuni kama hizo.
“Kuna baadhi ya kampuni za bima badala ya kutoa huduma bora kwa wananchi zimekuwa kilio,mfano mwananchi analipia kila kitu kwenye kampuni ya bima lakini anapopata majanga aidha ajali majanga ya moto inachelewesha kumpa fidia ,hivyo niagize TIRA ifuatilie suala hili ambalo imekuwa kero kwa wananchi.Kampuni moja ya bima ikiwa chafu imeharifu taswira ya makapuni mengine pia”alisema Dokta Mahenge.
Aidha,Dokta Mahenge amesema Tasnia ya Bima ina mchango mkubwa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi endapo itaendeshwa kwa kufuata miongozo na taratibu ya kisheria huku akitoa wito kwa makampuni ya bima kuendelea kutoa elimu kwa wananchi umuhimu wa bima hivyo ni wajibu kwa makampuni ya bima kutoa huduma nzuri na yenye viwango ili kuvutia wawekezaji makao makuu ya nchi,Dodoma.
Hata hivyo,Dokta Mahenge amesema ni Muhimu kwa makapuni yote ya Bima yakatoa huduma ya Bima ya Afya huku akitanabaisha kuwa serikali imeongeza bajeti ya dawa hospitalini kutoka Milioni 900 hadi Bilioni 4 kwa Mkoa wa Dodoma.
Kwa upande wake,Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima[TIRA]Kanda ya kati Bi.Stella Rutagiza amesema mwaka 2015 serikali ilianzisha ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Tanzania[Tanzania Insurance Ombundsmen] ambayo inaongozwa na Jaji Mstaafu Mhe.Vicent Lyimo ikiwa na lengo la kuwasaidia wananchi wake wenye migogoro ya Bima ili kuepuka gharama kubwa za kwenda mahakamani.
Aidha,Bi.Stella ametaja baadhi ya madhumuni ya maadhimisho ya siku ya Bima kanda ya kati kuunga mkono juhudi kubwa za Rais Mhe. John Pombe Magufuli kuinua uchumi wa nchi,kutoa elimu pamoja na kupanua wigo wa huduma za Bima.
Katika hatua nyingine Bi.Stella amebainisha baadhi ya Mafanikio ya TIRA ni pamoja na kuongezeka watoa huduma za Bima kutoka 10 mwaka 2015 na kufikia watoa huduma 27 mwaka 2019 pamoja na kupungua kwa malalamiko ya Bima kutoka kwa wananchi ambapo mwaka 2017kulikuwa na malalamiko 17,mwaka 2018 malalamiko 13 na kupokea malalamiko matatu pekee kwa mwaka 2019.
Maadhimisho ya siku ya Bima kanda ya kati tarehe 17-19/2019 yanaenda sambamba na kaulimbiu isemayo”Kata Bima,Inua Uchumi wa Nchi Yako”
Social Plugin