Kampuni ya Safaricom imemteua ofisa mtendaji mkuu wake wa zamani, Michael Joseph kukaimu nafasi ya mtendaji mkuu iliyoachwa na Bob Collymore aliyefariki dunia jana Julai 1, 2019.
Kwenye mkutano maalumu wa wakurugenzi jana Jumatatu, bodi ya kampuni imeamua kumteua Michael Joseph kuongoza ambapo utekelezaji unaanza mara moja.
“Joseph atashikilia wadhifa huo hadi pale kampuni itakapotoa tangazo jingine kuhusu uteuzi wa kudumu,” Safaricom ilisema kwenye taarifa yake.
Joseph ni mjumbe katika bodi ya Safaricom na ni mwenyekiti wa sasa wa Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways.
Mwili wa Collymore aliyechukua wadhifa huo kutoka kwa Joseph Novemba 2010, utazikwa leo jijini Nairobi katika tukio litakalohusisha tu wanafamilia.
Social Plugin