Serikali mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na Wadau wa afya (HPSS) wamezindua kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, ili waweze kupata huduma ya matibabu kwa gharama nafuu.
Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika leo Julai 16, 2019 kwenye kijiji cha Ilobashi kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa huo,Mhe. Zainab Telack, na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ya CHF iliyoboreshwa ,Telack amewataka wananchi wa mkoa wa Shinyanga wajiunge kwa wingi, ili pale wanapotatwa na magonjwa na kukutwa hawana fedha,kadi hiyo ya CHF itawawezesha kuwapatia matibabu bure bila ya kutoa gharama yoyote ile.
Amesema kadi hiyo ya bima ya afya CHF iliyoboreshwa inakatwa kwa bei ya Shilingi 30,000 kwa kila Kaya, ambapo watatibiwa watu sita kwenye kaya moja kwa muda wa mwaka mzima, ambapo matibabu watayapa kuanzia ngazi ya zahanati, kituo cha afya, wilaya, hadi hospitali ya mkoa.
“Naomba wananchi wa mkoa wa Shinyanga mjitokeze kwa wingi kujiunga kwenye mfuko huu bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kwani ni mkombozi kwetu , ambapo pale utakapougua japo atuombei kwani ugonjwa pia hua hauna hodi, utaweza kukusaidia kupata matibabu kwa gharama nafuu sawa na bure,”amesema Telack.
“Naagiza pia kwenye huduma zote za kiafya mkoani hapa zihakikishe madirisha yanakuwepo ya wagonjwa ambao wana kadi za CHF iliyoboreshwa, wapewe kipaumbele, pamoja na kupewa huduma stahiki yakiwamo na madawa, ili waweze kupata tiba na kuimarisha afya zao,”ameongeza.
Katika hatua nyingine amewataka wananchi kuachana na tabia ya kupenda kwenda kutibiwa kwa waganga wa kienyeji, bali waudhulrie kwenye vituo vya afya kupata tiba, ikiwa serikali imeboresha huduma hizo kwa kujenga vituo vya afya 11 pamoja na hospitali za wilaya mbili, sambamba na kuwepo kwa dawa za kutosha.
Naye Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga, amewataka wananchi wa mkoa wa Shinyanga hususani wakulima, pale watakapouza pamba yao wahakikishe wanatenga fedha kwa ajili ya kukata bima hiyo ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, ambayo itaswaidia kwenye matibabu pale watakapougua.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashidi Mfaume, ametaja takwimu za wananchi mkoani humo ambao wamejiunga na CHF iliyoboreshwa kuwa ni kaya 25,513 sawa na asilimi 9.8, kati ya kaya 261,608 idadi ambayo ni ndogo.
Meneja mradi wa HPSS tuimarishe afya Mkoani Shinyanga Dkt. Harun Kasale, amesema kutokana kuwepo kwa idadi ndogo ya wananchi mkoani humo kujiunga CHF iliyoboreshwa, kwa kushirikiana na Serikali ya Uswizi wameona ni vyema kuzindua kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na bima hiyo ambayo itawasaidia kwenye matibabu.
Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizindua kampeni ya kuhamasisha wananchi wa mkoa huo kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa ili kuwasaidia kupata matibabu kwa gharama nafuu.Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiunga na bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa ambayo itakuwa msaada mkubwa kwenye matibabu pale watakapougua na kukutwa hawana fedha.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack, akielezea namna Serikali inavyo boresha huduma za kiafya ambapo mpaka sasa vimeshajengwa vituo vya afya vipya 11 pamoja na hospitali za wilaya mbili, pamoja na kuwepo na madawa ya kutosha, na kuwataka wananchi wachangamkie fursa hiyo ya kukata bima ya afya CHF iliyoboreshwa ili waweze kufaidi huduma za matibabu kwa gharama nafuu.
Meneja mradi wa HPSS tuimarishe afya Mkoani Shinyanga Dkt Harun Kasale, akielezea kutokana kuwepo kwa idadi ndogo ya wananchi mkoani humo kujiunga na bima ya CHF
iliyoboreshwa, kuwa kwa kushirikiana na serikali ya Uswizi ndipo wakaona ni vyema kuzindua kampeni hiyo ya
kuhamasisha wananchi kujiunga na bima hiyo ambayo itawasaidia kwenye matibabu.
iliyoboreshwa, kuwa kwa kushirikiana na serikali ya Uswizi ndipo wakaona ni vyema kuzindua kampeni hiyo ya
kuhamasisha wananchi kujiunga na bima hiyo ambayo itawasaidia kwenye matibabu.
Waziri wa Kilimo.Mhe. Japhet Hasunga, akiwataka wananchi wa mkoa wa Shinyanga pale watakapouza Pamba yao wahakikishe wanatenga fedha kwa ajili ya kukata kadi ya bima hiyo ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa ambayo itawasaidia kupata matibabu kwa gharama nafuu pale watakapougua na kukutwa hawana fedha za matibabu.
Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga akielezea umuhimu wa mwananchi kuwa na afya njema, ambapo mwananchi akiwa na afya yenye mgogoro kamwe hataweza kujihusisha na shughuli za kiuchumi kikiwamo kilimo na hatimaye kushindwa kukua kimaendeleo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akisisitiza wananchi kujiunga na bima ya CHF iliyoboreshwa ambayo itakuwa msaada mkubwa kwenye upataji wa matibabu yao kwa gharama nafuu ambapo kaya wenye watu sita wataweza kutibiwa mwaka mzima kwa shilingi 30,000.
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akitoa takwimu za mkoa huo kwa kaya ambazo zimejiunga na CHF iliyoboreshwa kuwa ni kaya 25,513 sawa na asilimia 9.8, kati ya kaya 261,608 idadi ambayo amebainisha kuwa ni ndogo.
Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, akimkaribisha mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, kuzungumza na wananchi kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa.
Wiliam Gwisu mkazi wa kijiji cha Ilobashi kata ya Masengwa Shinyanga, akielezea namna anavyonufaika na kadi hiyo ya bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa ambapo hua anapata matibabu bure kabisa bila ya kutoa hata shilingi.
Salu Izengo ni Mwananchi wa kijiji cha Bubale Kata ya Masengwa Shinyanga , akielezea naye namna anavyofaidika na kadi hiyo ya bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, nakutoa wito kwa wananchi wenzake wajiunge ikiwa inafaida kubwa sana kimatibabu.
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya hamasa ya kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kikoa ambayo imezinduliwa kwenye kijiji cha Ilobashi kata ya Masengwa Shinyanga.
Wananchi wa kata ya Msengwa wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya hamasa ya kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, wakisikiliza umuhimu wa bima hiyo ambayo itawasaidia kupata matibabu kwa gharama nafuu, kwa shilingi 30,000 ndani ya mwaka mzima kwa Kaya yenye watu sita.
Uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi mkoani Shinyanga kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa ukiendelea katika kijiji cha Ilobashi kata ya Masengwa.
Wananchi wa Kata ya Msengwa Shinyanga vijijini wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya hamasa ya kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF
iliyoboreshwa, wakisikiliza umuhimu wa bima hiyo.
iliyoboreshwa, wakisikiliza umuhimu wa bima hiyo.
Wananchi wa Kata ya Msengwa Shinyanga vijijini wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya hamasa ya kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF
iliyoboreshwa, wakisikiliza umuhimu wa bima hiyo.
iliyoboreshwa, wakisikiliza umuhimu wa bima hiyo.
Wananchi wa Kata ya Msengwa Shinyanga vijijini wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya hamasa ya kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa
Kikundi cha ngoma kutoka kijiji cha Bubale Kata ya Masengwa wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ya kuhamasisha wananchi wa mkoa wa Shinyanga kujiunga na mfuko huo wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, ili kuwapatia matibabu kwa gharama nafuu.
Wanafunzi kutoka Shule ya msingi Ilobashi kata ya Masengwa wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ya bima ya afya CHF iliyoboreshwa.
Meza kuu ikiangalia burudani kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi wa mkoa wa Shinyanga kujiunga kwenye mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa.
Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko wakicheza na Jeshi la Jadi Sungusungu la kijiji cha Ilobashi kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya CHF iliyoboreshwa.
Awali Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga akiwasili na mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telackkwenye uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi wa mkoa wa Shinyanga kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa , uzinduzi uliofanyia kwenye kijiji cha Ilobashi Kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Social Plugin