Klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam imetangaza kumsajili Fransis Kahata ambaye msimu uliopita alikuwa anakipiga na timu ya Gor Mahia ya Nchini Kenya.
Akiwa na Klabu hiyo alishinda Kombe la Ligi Kuu mara tatu, kiungo bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Kenya mara mbili na mchezaji bora wa msimu 2018/2019 wa Gor Mahia.
Fransis Kahata akisaini mkataba na Simba Sc
Taarifa ambayo imetolewa na Wekundu hao wa msimbazi saa majira ya saa 11 jioni kupitia ukurasa wao wa Instagram Simba imeingia mkataba wa miaka miwili na Kahata na atavaa jezi namba 27.
Kahata ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kucheza eneo la kiungo, kwasasa ni sehemu ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars kinachoshiriki Afcon.
Social Plugin