Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAKUKURU DODOMA YAIBUA MADUDU MRADI WA MAJI KELEMA

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuru mkoa wa Dodoma imeingilia kati ujenzi wa mradi wa maji wa kijiji cha kelema kuu wilayani chemba  baada ya kubaini thamani ya fedha iliyotumika kutoendana na kazi halisi na kuokoa shilingi  Milioni  67 ,laki   5,42 elfu na mia 600.

Akitoa  taarifa ya robo ya nne    ya TAKUKURU  kwa waandishi wa habari ya kuanzia  Mwezi April  hadi Juni 2019, mkuu wa TAKUKURU  mkoa wa Dodoma Bw Sosthenes Kibwengo amesema kuwa hatua hiyo imefanyika ikiwa ni utekelezaji wa majukumu ya Takukuru chini ya kifungu cha saba [7] cha sheria ya kuzuia na kupamabana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 .

Mradi huo wa maji unagharimu kiasi cha Tsh.milioni 222,laki 9,elfu 78,mia 680 na ulipaswa kukamilika tangu mwaka 2015.

“TAKUKURU mkoa wa Dodoma  imeingilia kati mradi wa maji  Kelema Juu,baada ya kubaini fedha iliyotumika kutoendana hali halisi na kazi iliyofanyika na uwekaji mabomba ukiwa chini ya kiwango hali iliyosababisha kutotoa maji na malipo yakiwa zidifu  tofauti na makubaliano ya mradi na kuanzia tarehe 1,julai anaanza kurudia kuifanya  kazi”

Aidha,Bw.Kibwengo amesema TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kuokoa na kurejesha serikalini  Tsh.Milioni  11 laki 88,77elfu,mia 353  zilizolipwa bila utaratibu kama mshahara kwenye akaunti  ya mwalimu aliyekuwa amefariki.

Katika hatua nyinyine bw Kibwengo amesema kuwa wamefanikiwa  kumkamata Bw Gaston Meltus Francis amabaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Global Space East Africa Limited iliyopewa kazi ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Mima wilayani mpwapwa baada ya kubaini kampuni hiyo kulipwa isivyo halali kiasi cha shilingi milioni 86 laki nne na tano na mia mbili na tano kwa kazi ambazo hazikufanyika katika mradi huo.
                                 
Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoa, Bw Kibwengo ameongeza kuwa TAKUKURU imefanya uchambuzi wa mifumo mbali mbali ya utendaji na utoaji wa huduma ili kubaini m  ianya na kushauri namna bora ya kuondokana nayo kwa lengo la kudhibiti vitendo vya rushwa huku pia ikitoa elimu kwa jamii  juu ya rushwa na kuzindua vilabu 39 ngazi ya shule na vyuo katika mapambano dhidi ya rushwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Sanjari na hayo, TAKUKURU mkoa wa Dodoma imefuatilia na kukagua miradi 34 yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 32 milioni 545 laki nne na elfu kumi na nane mia moja na kumi na sita ambapo asilimia 95.4 ya matumizi ya fedha za miradi hiyo ikionekana kufanyika vizuri.

Hata hivyo ,TAKUKURU Mkoa wa  Dodoma imebaini viashiria vya jinai katika miradi minnne ambapo TAKUKURU inafanya uchunguzi uhalali wa malipo   katika miradi hiyo kiasi  cha Tsh.bilioni 1 ,milioni 409 na laki 9 yaliyofanyika katika miradi hiyo ambayo ipo katika sekta  ya za ujenzi ,Afya,Elimu na Kilimo.

Katika taarifa ya TAKUKURU ya  robo za Jauari,Machi hadi Juni Mwaka huu ,TAKUKURU mkoa wa Dodoma ilipokea taarifa135 za Rushwa na Makosa mengineyo katika michanguo ifuatayo  ambapo,ardhi asilimia ,36%,serikali  za Mitaa asilimia 31%,Polisi asilimia 8%,Kilimo  asilimia 6%,mahakama na ujenzi kila moja asilimia 4%,asilimia 11% zilizobaki ni katika sekta za   ,Afya,maji,Madini,Ukusanyaji mapato huku ikiendelea na Mashauri  30 mahakamani hadi sasa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com