Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAKUKURU SHINYANGA YAANZA MIKAKATI KABAMBE KUDHIBITI RUSHWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga imeanza mkakati kabambe kukabiliana na vitendo vya rushwa katika kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 11,2019, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga, Hussein Mussa katika mikakati yao ya utendaji kazi kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2019 wanatoa elimu ya rushwa kwa wananchi (wapiga kura na wale wataogombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa).

"Elimu tunayotoa inahusu makosa ya rushwa,sheria za gharama za uchaguzi kama zilivyoainishwa na sheria ya gharama za uchaguzi Na.6 ya mwaka 2010 na Makosa yaliyopo kwenye sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007",alisema.

"Natoa rai kwa wagombea wote katika uchaguzi wa mwaka huu kuwa makini na mienendo yao ya kuhakikisha kwa namna yoyote hawajihusishi na vitendo vyovyote kinyume na sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007 pamoja na sheria ya gharama za uchaguzi kama zilivyoanishwa na sheria ya gharama za uchaguzi Na. 6 ya mwaka 2010",aliongeza Mussa.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com