Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANZANIA YADHAMIRIA KUPUNGUZA MATUMIZI YA ZEBAKI KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI YA DHAHABU KWA ASILIMIA 30% IFIKAPO 2024


Katika kikao cha kupitisha Mpango Kazi wa Taifa wa kupunguza matumizi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo kilichoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kushirikisha sekta husika, jana katika Chuo cha Biashara (CBE) jijini Dodoma, Ikiwa sehemu ya Maandalizi ya utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Minamata ambao Tanzania ipo kwenye mchakato wa kuridhia.

Zebaki imetajwa kuwa moja kati ya kemikali kumi hatarishi zilizo orodheshwa na Shirika la Afya Duniani na ina madhara makubwa haswa kwenye magonjwa ya mfumo wa fahamu.

Tanzania inakadiriwa kuwa na wachimbaji wadogo milioni 1.2, asilimia 20-30 ni wachimbaji wanawake ambapo sehemu kubwa ya wachimbaji hawa hutumia zebaki huku kukiwa na makisio ya mwaka ambapo tani 13 mpaka 24 hutumika na huingizwa nchini kinyemela.

Zaidi ya 25-33% ya wachimbaji wadogo wadogo wameathirika na matumizi ya zebaki,hivyo Serikali imedhamiria kupunguza  ama kuondosha matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo.

Wakizungumza mara baada ya kumaliza kikao hicho Bi. Noela R. Magoche ambaye ni mdau wa Madini alisema kuwa zifikiriwe mbinu mbadala kunusuru watoto wanaofanya kazi migodini kwani ndio waathirika wakubwa wa zebaki huku akisisitiza sheria inayokataza  ajira kwa watoto

Kwa upande wake mdau wa Mazingira Bw. Haji Rehani amesema zebaki imetambulika kimataifa kwa madhara makubwa ya kiafya.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com