Mwenyekiti wa kamati ya taifa ya Uongozi ya TASAF,Dr.Moses
Kusiluka (aliyesimama) akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Ludilo wilaya ya Mfindi mkoani Iringa juu ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William na kulia kwake ni Meneja wa Ukaguzi wa Ndani wa TASAF Shadrack Mziray.
Dkt.Kusiluka ( picha ya juu na chini ) akiwa katika shamba la parachichi la Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Ludilo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa wa TASAF Dr.Moses Kusiluka picha ya juu na chini akikagua mabwawa ya samaki yaliyochimbwa na Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Ludilo wilayani Mufindi mkoani Iringa kupitia utaratibu wa ajira ya muda.
Dr.Moses Kusiluka (wanne kutoka kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Walengwa wa TASAF na viongozi wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Baadhi ya Walengwa wa TASAF wakisikiliza nasaha za Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya Mfuko huo katika kijiji cha Ludilo wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Ludilo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wakitoa burudani baada ya kuwasili kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Ikulu Dr. Moses Kusiluka kukagua utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF.
Na Estom Sanga-Njombe
Wananchi wanaonufaika na huduma za serikali kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAFwameaswa kutumia vizuri huduma hizo ili waweze kuboresha maisha yao na kupambana na umaskini.
Akizungumza na Walengwa wa Mpango huo katika kijiji cha Ludilo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi wa Mfuko huo Dr. Moses Kusiluka amesema serikali imedhamiria kwa dhati kupunguza adha ya umaskini miongoni mwa Wananchi wake hivyo akataka wananchi na wadau wengine kuunga mkono jitihada hizo.
Dr.Kusiluka amesisitiza umuhimu wa Walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini kuendelea kutumia huduma za TASAF kwa kuanzisha miradi itakayowawezesha kujiongezea kipato na hivyo kuwa na uwezo mzuri zaidi wa kuhudumia familia zao na kupunguza umaskini.
Aidha Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF ambaye pia ndiye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Ikulu, amesema utekelezaji wa Mpango huyo ni wa Serikali na Wadau wengine wa Maendeleo ambao wanaendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa kuchangia fedha na ushauri mwingine wa kitaalamu.
Akiwa katika kijiji hicho Dr. Kusiluka ameshudia miradi ya kilimo cha miti ya matunda ya parachichi, maharage na mabwawa ya samaki ambayo inatekelezwa na Walengwa wa TASAF kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda na kuonyesha kuridhishwa na miradi hiyo ambayo inawaongezea kipato Walengwa hao.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Mufindi, Jamhuri William amepongeza jitihada za serikali kupitia TASAF katika kuchochea kasi ya maendeleo wilayani humo ambazo amesema zimeibua hamasa kubwa ya Wananchi kuboresha maisha yao hususani katika sekta ya makazi,elimu,Afya ,kilimo,mifugo ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya kuanza kwa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini.