Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TATIZO LA UCHELEWESHWAJI WA MIZIGO BANDARI YA DAR ES SALAAM KUPATIWA UFUMBUZI


WAZIRI wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwele amesema kuwa Rais John Magufuli ametoa fedha nyingi za matengenezo ya miundombinu ya bandari na reli hali iliyopelekea watumiaji wa reli na bandari ya Dar es Salaam kutoka nje kusifia uimarikaji wa mfumo huo ambao unarahisisha upitishwaji wa mizigo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijiji Dar es Salaam mara baada ya kukutana na wafanyabiashara wa kimataifa wanaotumia bandari ya Dar es Salaam Kamwele amesema kuwa watumiaji wa muindombinu hiyo wamesema kuwa Kuna faida kubwa katika biashara yao licha ya changamoto ya ucheleweshwaji wa mizigo ambayo inapatiwa ufumbuzi kujitokeza mara kwa mara.

Amesema kuwa wafanyabiashara hao wamesema kuwa Sera na sheria ziboreshwe jambo ambalo amewahaidi kukaa na mamlaka husika ili kutatua changamoto zinazoikumba sekta hiyo.

Mhandisi Kamwelwe amesema kuwa baada ya mwezi mmoja watakaa tena na wafanyabiashara hao na kuangalia zaidi namna ya kuitumia vyema bahari ya Hindi na wizara hiyo itakaa na wamiliki wa meli duniani ili kuboresha zaidi uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini (TPA) Mhandisi Deusdetit Kakoko amesema kuwa watumiaji wa bandari hiyo wakiwemo wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo wategemee makubwa kupitia bandari hiyo ambapo hadi sasa miundombinu ya tehama na ulinzi vinaimarishwa zaidi.

 Kuhusiana na sera na sheria Kakoko amesema kuwa ushirikiano baina ya wizara hiyo na wizara ya fedha itazaa matunda kwa manufaa ya taifa na watumiaji wa bandari hiyo.

Pia amewataka wadau wateja na mamlaka husika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano pamoja  na kushirikiana ili kuipeleka nchi katika uchumi wa Kati.

Mwisho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com