Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI


Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amefutilia mbali uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona, Philippe Coutinho, 27, ambaye aliondoka Anfield kwa kima cha £142m mwaka 2018. (ESPN)

Paris St-Germain imekubali kulipa £28m kumsajili kiungo wa kimataifa wa Senegal Idrissa Gueye, 29, kutoka Everton. (Mail)

Toffees wanaendelea kushauriana na Crystal Palace kuhusu usajili wa nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, kwa pauni £80m. (Sky Sports)

Tottenham imewasiliana na Juventus kuhusu usajili wa nyota wa kimataifa wa Argentina international mshambuliaji Paulo Dybala, 25, ambaye bei yake anayekadiriwa kuwa £80m. (Evening Standard)Paolo Dybala

Manchester United wameomba kufahamishwa kuhusu hatma ya mchezaji Christian Eriksen, 27, wa Tottenham. Kandarasi ya nyota huyo wa kimataifa wa Denmark amesalia na mwaka mmoja kukamilika na huenda akauzwa kwa pauni milioni 70. (Mail)

United pia inamlenga mshambuliaji wa Lille na nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Nicolas Pepe, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £70m, kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku endapo atajiunga na Inter Milan. (Times)Romelu Lukaku aliifungia United mabao 15 msimu uliopita

Kiungo wa kati wa Kimataifa wa Serbia na Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 24, amewaambia wachezaji wenzake kuwa ataondoka klabu hiyo msimu huu licha ya tetesi huendaakajiunga na Manchester United. (Il Tempo via Express)

Chelsea na West Ham wanapania kumsajili kwa mkopo winga wa Portsmouth Leon Maloney, 18 ambaye ameifungia Pompey academy mabao 26 msimu uliopita. (Sun)

Wolfsburg na RB Leipzig wanataka kumsajili kwa mkopo winga wa Arsenal wa miaka 18 Muingereza Emile Smith Rowe. (Independent)Emile Smith-Rowe

Crystal Palace na Aston Villa wanataka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland anayecheza safu ya mashambulizi Jonathan Afolabi ambaye aliondoka Southampton mwisho wa msimu uliopita. (Football.London)

Sheffield United ambao wamepandishwa daraja kushiriki ligi kuu ya Premia wanatafakari uwezekano wa kumnunua kipa wa zamani wa kimataifa wa England Joe Hart, 32, kutoka Burnley. (Mail)Kipa wa Burnely Joe Hart

Villa wanashauriana na kipa wa Juventus, Mtaliano Mattia Perin baada ya uhamisho wake £13m kwenda Benfica kugonga mwamba baada ya kukosa uchunguzi wa kiafya. (Football Italia)

Barcelona wameweka dau la £24m kumnunua mlinzi wa Real Betis na Uhispania Junior Firpo. (Sport - in Spanish)

CHANZO.BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com