Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera (wa pili kulia) akimkabidhi Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi Benjamini Kuzaga(wa nne kulia) msaada wa vigae vya sakafuni vyenye thamani ya Shilingi milioni nane zilizotolewa na benki ya Posta Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari wa wilaya ya Mpanda mkoani humo. Picha na Walter Mguluchuma - Malunde1 blog Katavi
Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Benjamin Kuzaga akimshukuru kwa kushikana mkono na Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi baada ya benki hiyo kukabidhi msaada wa vigae vya sakafuni vyenye thamani ya shilingi milioni nane kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari wilaya ya Mpanda.
Na Walter Mguluchuma - Malunde1 blog Katavi
Benki ya Posta TPB imetoa msaada wa vigae 290 vya sakafu kwa jeshi la Polisi Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi vyevye thamani ya shilingi milioni nane ili visaidie ujenzi wa nyumba za askari zinazoendelea kujengwa wilayani Mpanda.
Msaada huo umekabidhiwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya polisi Katavi ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera.
Akikabidho vigae hivyo, Mkurugenzi mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi alisema benki yake ina amini kwamba jeshi la polisi ni wadau wake wakubwa katika kuhakikisha ulinzi na usalama kwa wateja wake na wananchi wote kwa ujumla wake .
Hivyo wameona ni muhimu kuwasaidia ili waweze kuishi kwenye makazi bora na waweze kufanya kazi zo kwa ufanisi mkubwa kwani biashara ya benki inategemea sana uwepo wa jeshi la polisi.
Moshingi alisema ili kuhakikisha matawi yao yanakuwa salama pia ulinzi pia ulinzi na usalama wa wateja wao na fedha zao zinakuwa salama unategemea sana uwepo wa jeshi la polisi hivyo polisi ni wadau wao muhimu katika biashara yao.
Moshingi alieleza kuwa, pia jamii inapokuwa na utulivu na salama ni rahisi kupiga hatua za kimaendeleo kwani bila usalama wananchi hawawezi kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Moshingi alisema wametenga kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajiri ya kusaidia maendeleo ya jamii kutokana na benki hiyo kuwa imepiga hatua kubwa,walianza wakiwa na matawi 36 na sasa wanato matawi 76 nchi nzima.
Alifafanua kuwa benki hiyo ilikuwa ikipata faida ya zaidi ya shilingi milioni 800 lakini mwaka jana wameweza kupata faida ya shilingi bilioni 17 hiyo inaonyesha ni jinsi gani walivyopiga hatua.
Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Benjamini Kuzaga aliishukuru benki ya TPB kwa msaada huo uliokuja kwa wakati muafaka kipindi ambacho jeshi la polisi likiwa kwenye mchakato wa kumalizia wa ujenzi wa nyumba za maaskari wake.
Alipongeza benki hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kwa kuonyesha ushirikiano wa jeshi hilo mara tu walipoombwa kufanya hivyo hivyo jeshi hilo limefarijika sana kwani vigae hivyo vitakwenda kukamilisha ujenzi wa nyumba za askari na kuwapatia makazi yenye hadhi wao na familia.
Kuzaga alisema wataendelea kutoa ushirikiano kwa benki ya hiyo kama ambavyo wamekuwa wakifanya na kutoa wito kwa wadau wengine waige mfano wa TPB kwa waliyoyafanya kwa jeshi la polisi Katavi .
Kamanda Kuzaga alisema jeshi la polisi linatarajia kujenga nyumba 20 za askari wake ambapo askari zaidi ya asilimia 90 wanaishi kwenye nyumba za kupanga mitaani na kubainisha kuwa katika mwaka wa fedha 2018/ 2019 walipokea kiasi cha shilingi milioni 500 ambazo ni sehemu ya ahadi aliyoitoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli kama mchango wa ujenzi wa nyumba hizo.
"Baada ya kukamilika kwa nyumba hizo zinatarajia kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa makazi kwa askari waliopo katika wilaya ya Mpanda ambapo kati ya nyumba hizo 20 nyumba 12 zinajengwa katika wilaya ya Mpanda na Wilaya za Tanganyika na Mlele wanajenga nyumba nne nne hivyo kufanya jumla ya nyumba 20 zitakazojengwa kwa mkoa wa Katavi",alieleza.
Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera alisema msaada huo ni mkubwa kwa jeshi la polisi na kwa wanachi wa mkoa huo na inaonyesha jinsi ambavyo benki hiyo inavyowajali watu wa pembezoni.
Alisema wakazi wa mkoa huo bado wanauhitaji mkubwa wa benki hiyo kwani kwa sasa benki ya TPB imeungana na benki ya wakulima hivyo waongeze matawi zaidi katika mkoa wa Katavi.
Social Plugin