Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki TPB Sabasaba Moshingi kulia akimkabidhi madawati hamsini (50),meza ya ofisi pamoja na viti, vitakavyotumiwa na wanafunzi pamoja na waalimu na vitasaidia kupunguza uhaba uliopo wa madawati shule ya Msingi Pongwe Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki TPB Sabasaba Moshingi kulia akimkabidhi madawati hamsini (50),meza ya ofisi pamoja na viti, vitakavyotumiwa na wanafunzi pamoja na waalimu na vitasaidia kupunguza uhaba uliopo wa madawati shule ya Msingi Pongwe Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Ramadhani Possi.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katikati akiwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki TPB Sabasaba Moshingi kulia wakiwa wamekaa kwenye madawati mara baada ya kuyapokea kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Ramadhani Posi na kulia ni Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi.
BENKI ya TPB imetoa msaada wa madawati na samani za ofisini kwenye shule ya msingi Pongwe Mkoani Tanga ikiwa ni kupunguza uhaba uliokuwepo awali.
Madawati hayo hamsini (50),meza ya ofisi pamoja na viti, vitavyotumiwa na wanafunzi pamoja na waalimu na vitasaidia kupunguza uhaba uliopo wa madawati shuleni hapo.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi madawati hayo shuleni hapo, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sabasaba Moshingi alisema benki hiyo ilipokea maombi kutoka uongozi wa shule ya msingi Pongwe ukiomba benki hiyo isaidie kutatua pamoja na changamoto nyingine, uhaba wa madawati na samani kwa ajili ya shule hiyo.
“Benki ya TPB inaipa sekta ya elimu umuhimu mkubwa, kwa kuiweka juu katika vipaumbele vyake kwenye sera zake za msaada kwa jamii ( Corprate Social Responsibility). Kila mwaka benki inafanya miradi mingi zaidi kwenye sekta ya elimu kuliko maeneo mengine inayoyaangalia”, alisema Moshingi.
Akipokea msaada huo, Mkuu wa Shule ya Msingi Pongwe Mwalimu Yahya Ally Mafita aliipongeza benki ya TPB kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitoa kwa sekta ya elimu nchini, hususan kwenye shule hiyo ya Pongwe.
Alisema shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo uhaba wa madawati, samani za ofisi ya waalimu zikiwamo meza na makabati ya kuhifadhi vitabu.
“Msaada huu utapunguza uhaba wa madawati uliokuwa ukitukabili, hivyo tunaishukuru sana benki ya TPB. Shule yetu ilipata bahati ya kujengewa madarasa matatu na taasisi ya TAWAH hapo mwaka jana, hivyo madawati haya kutoka benki ya TPB yatakwenda kutumika ndani ya madarasa hayo”, alisema mwalimu Mafita.
Naye kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini Mhe. Thobias Mwalipwa aliishukuru benki ya TPB kwa msaada huo, na kusema kwamba utaisaidia kupunguza changamoto kubwa ya madawati pamoja na samani iliyokuwa ikiwakabili.
Alisema shule inapokuwa na madawati pamoja na vifaa vingine vinavyohitajika hujenga ari ya kujifunza kwa wanafunzi na kutoa motisha kwa walimu ili waweze kufundisha vizuri katika mazingira bora.