Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imevifungulia vyuo ambavyo vilifungiwa udahili kikiwemo Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji, Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian Bagamoyo, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), na Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu Mihayo (AMUKTA).
Akizungumza wakati wa Maonyesho ya TCU yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jana Jumatatu Julai 15, 2019, Mkurugenzi wa Uratibu na Udahili wa tume hiyo, Dk Kokuberwa Katunzi-Mollel alisema vyuo hivyo vimeruhusiwa kufanya udahili baada ya kukidhi vigezo vilivyotakiwa.
Tayari dirisha la udahili kwa mwaka huu limefunguliwa kwa awamu ya kwanza kuanzia jana Jumatatu Julai 15 hadi Agosti 10, 2019, hivyo akawataka wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu kuanza kutuma maombi.