Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola jana alishindwa kujizuia na kuamua kwenda kuungana na Bendi ya polisi nchini Tanzania kusakata muziki na kuonyesha naye ni mjuzi wa kucheza hali iliyoibua shangwe kutoka kwa watu waliohudhuria shughuli hiyo.
Tukio hilo lilitokea jana Jumatatu July 15 wakati wa hafla ya ufunguzi wa nyumba 20 za polisi eneo la magogo mjini Geita.
Uzinduzi huo ulifanywa na Rais wa Tanzania, John Magufuli ambapo bendi hiyo ilionyesha uhodari wake wa upigaji mzuri wa tarumbeta uliombatana na mbwembwe za wapigaji ulikuwa kivutio kilichowafanya viongozi washindwe kuvumilia kukaa kwenye viti na kushuka kutoka jukwaa kuu na kwenda kuwatunza
==>>Tazama Video Hapo Chini