Na Amiri kilagalila-Njombe
Waziri wa nishati dkt.Medard kalemani ametoa maelekezo kwa shirika la umeme Tanzania Tanesco kuhakikisha linafikisha baadhi ya mitambo ya kisasa kwa wagunduzi wa umeme walioibuliwa hivi karibuni mkoani Njombe ili kuweza kuongeza uzalishaji wa nishati katika vyanzo vyao.
Waziri kalemani ametoa maelekezo hayo mkoani Njombe alipotembelea mitambo ya kuzalishia umeme kwa wagunduzi John fute (Mzee pwagu) wa Msete pamoja na bwana Lainery Ngailo wa Lugenge mjini Njombe mkoani humo.
“Mfano nilivyoiona haraka ile pressure ya maji hapa kwa mzee Fute ni kubwa sana sio ya kutumia tu kupata kilowati 28 tunaweza tukapata hata megawati moja,na megawati 1 inaweza ikahudumia wananchi zaidi ya 800 mpaka 1000 hata kata nne,ukiangalia Burundi wana megawati 45 za umeme na wanahudumia nchi nzima”amesema Kalemani
Waziri kalemani ameongeza kuwa
“Tanesco wanachotakiwa ni kushirikiana na huyu bwana ili kusudi waanze kujenga ile kingo,waweke transfoma tuone pa kuanzia kama mfano pamoja na kumsaidia Tabani,tunaweza kufanya kama project kwa mwaka mmoja lakini wakati huo mwaka mmoja wananchi majirani wa hapa wakatumia huo umeme bure ili kutazama hali itakavyo kuwa”amesema Kalemani
Awali wagunduzi hao akiwemo mzee John fute alisema,umeme anaouzalisha anautumia kwaajili ya matumizi yake nyumbani lakini hata hivyo amesimamisha huduma za usagaji wa nafaka kutokana na kufunga tabani ndogo huku mzee Ngailo naye akishukuru kwa uamuzi wa waziri.
“mfano mimi nilikuwa nawasaidia hata majirani kusaga unga kwa shilingi mia tano,lakini kwa sasa nimefunga kutokana na kufunga tababani ndogo,na mimi hapa kwenye chanzo changu kuna kama kilowati 300 hivi ambazo kwa kuanzia ninaweza kuwasambazia kama watu 600 hivi lakini kwa sasa hivi ninazalisha chini ya kilowati 28”alisema Mzee pwagu
Hata hivyo licha ya wagunduzi hao kukabidhiwa fedha kiasi cha shilingi milioni 15 kila mmoja siku chache zilizopita na shirika la umeme Tanzania tanesco kutokana na ahadi iliyotolewa mbele ya Rais Magufuli,shirika limeweza kusimika jumla ya Nguzo sabini,kurekebisha mashine,kufunga nyaya mpya pamoja na vikombe kutoka kwenye chanzo cha umeme cha mzee Ngailo na kughalimu takribani milioni 100.