NA AVITUS BENEDICTO KYARUZI , KAGERA
Rais wa jamhuli ya muungano wa Tanzania Dr john Pombe Magufuri ametoa kibali kwa wanunuzi wa zao la kahawa kutoka nje ya nchi kuingia mkoani kagera kufanya biashara ya zao hilo.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo july 11 mwaka huu wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Kyaka wilayani Misenyi alipo kuwa akitokea wilayani karagwe akielekea wilayani Chato Mkoani Geita
Rais Magufuli amesema kuwa zao la kahawa mkoani Kagera kwa kipindi cha Nyuma wakulima wa zao hilo wamekuwa wakiuza kahawa zao kwa bei ya chini na kuwalazima kuuza kahawa Hizo Kwa magendo ambapo gunia moja lilikuwa ni elfu 30 ambapo kwa sasa limepanda bei hadi kufikia elfu 80.
Dokta Magufuli amesema kuwa sasa ni muda kwa wanunuzi mbali mbali kutoka nje ya nchi kuingia mkoani Kagera ili kuanza ununuzi wa zao hilo.
Sambamba na hayo Rais Magufuli amemwagiza mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia jenerali Marcko Elisha Marco Gaguti kuhakikisha vyama vyote vya ushirika vya mkoani hapa wanawalipa wakulima fedha zao ndani ya siku saba wanapochukua kahawa yao kwenye vyama vya msingi vyote vinavyo kusanya kahawa hizo.
Pia Rais Magufuli amemwangiza Mkuu wa Mkoa wa kagera kuhakikisha wafanya baashara wa kahawa wanaotoka nje ya Tanzania wananunua kahawa ya mkulima kwa zaidi ya shilingi elfu moja na mia moja za kitanzania.
Hata hivyo Rais Magufuli amewahakikishia wakulima wa zao la kahawa kuacha magendo kwani serikali ipo bega kwa bega na wakulima hao ili kuhakikisha wanapata malipo yao ya awamu ya pili baada ya mauzo ya kahawa hizo zitakazo kusanywa na vyama vyote vya msingi na kuuzwa kwenye soko la dunia.
Social Plugin