Waziri wa Viwanda na Biashara ,Innocent Bashungwa amekemea baadhi ya Watanzania wanaopotosha na kukandia kuwa korosho ya Tanzania iliyopo kwenye maghala ,haina ubora ambapo amewapasha kuacha propaganda zisizo na tija kwa Taifa.
Ameyasema hayo mjini Kibaha alipotembelea kiwanda cha Kubangua Korosho cha Terra Cashew na kiwanda cha sabuni ya unga cha Keda vilivyopo wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Bashungwa alisema kuwa korosho ya Tanzania ni bora na iko kwenye daraja la kwanza na la pili huku daraja la tatu likiwa ni kidogo sana.
“Tunaitangazia dunia kuwa korosho ya Tanzania ina ubora na viwango vinavyotakiwa na katika kuhakikisha ubora huo nimepita kwenye maghala yote 37 ambayo yanahifadhi korosho nikiwa na wataalamu tumehakiki na kujionea hali halisi,” alisema Bashungwa.
Alisema kuwa wameandaa taarifa za kila ghala na aina na ubora wa korosho hivyo wanunuzi wanaweza kupata taarifa zote juu ya korosho na aina wanayoitaka.
Social Plugin