Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMII YATAKIWA KUTOWATENGA WATU WENYE ULEMAVU


Jamii imetakiwa kutowabagua wala kuwanyanyapaa watoto wenye ulemavu badala yake wapewe vipaumbele na mahitaji muhimu ili wajione sawa na watu wengine.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu waTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kagera John Joseph wakati akiongea na Malunde 1Blog ofisini kwake.

Joseph amesema kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwatenga, kuwabagua watu wenye ulemavu wakiwemo watoto jambo ambalo husababisha makundi hayo kujiona ni watu wa tofauti katika jamii.

Mkuu huyo amesema ili kulipa uzito suala hilo Julai 28 mwaka huu wanafunzi wa shule ya Sekondari Kahororo iliyoko mkoani Kagera kwa kushirikiana na taasisi hiyo watakwenda kutembelea shule ya wanafunzi walemavu katika shule sekondari Mgeza Mseto kwa ajili ya kuwapelekea mahitaji mbalimbali.

Amesema makundi ya watu wenye ulemavu ni sehemu ya jamii na ili makundi hayo yatambue kuwa jamii haijawatenga ni vyema kila mmoja ashiriki katika kuwatembelea kuwajali na kuwapa chochote walemavu waliopo katika maeneo yao.

Amesema katika ushiriki wa makundi ya vijana juu ya mapambano dhidi ya Rushwa, taasisi hiyo imefanikiwa kuyaelisha makundi ya wanafunzi kwa kuanzisha Klabu za wapinga rushwa shuleni.
Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog Kagera

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com