MITANDAO YA WHATSAPP, INSTAGRAM NA FACEBOOK YAKUMBWA NA TATIZO....FACEBOOK YAOMBA RADHI



Mitandao ya Kijamii ya Facebook,Instagram na Whatsapp imekumbwa na tatizo la kiufundi siku ya Jumatano Julai 3,2019 ambapo watumiaji wake kutoka maeneo mbalimbali duniani wanashindwa kupakia au/na kupakua picha,video na jumbe za sauti. 

Baadhi ya watumiaji wa Facebook, Instagram na WhatsApp walishindwa kuweka picha, video na mafaili.

Facebook, inayomiliki App zote tatu, imesema inafahamu kuhusu tatizo hilo na ilikuwa ''ikifanyia kazi ili kurudisha kila kitu sawa haraka iwezekanavyo''.

Mitandao ya kijamii, ina mabilioni ya watumiaji wake ulimwenguni.

Washindani wake Twitter pia walikuwa na tatizo kwa watumiaji wake kushindwa kutuma ujumbe wa moja kwa moja au kupokea taarifa kuhusu ujumbe ulioingia.

Kampuni iliomba radhi kwa dosari hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter wakisema kuwa wanashughulikia tatizo hilo.

Watumiaji bado waliweza kuweka ujumbe kwenye twitter na ujumbe wa hashtag #instagramdown ukaanza kushika kasi mtandaoni wengi wakitumia kueleza matatizo ya mshindani wake.

App ya Facebook Messenger, ambayo huwa inapakuliwa kivyake, nayo ailiathirika.

Mwezi Machi, Facebook na Instagram ilipata changamoto za kiteknolojia ambayo ilidumu wa muda. Matatizo pia yalikumba app zote mbili sambamba na Whats App mwezi Aprili.

Facebook ina watumiaji zaidi ya bilioni 2.3 kwa mwezi wanaotumia app hiyo na Instagram ina watumiaji bilioni moja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post