Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Meneja Mawasiliano wa asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Bi. Agnes Kabigi aliyefariki dunia jana Julai 26,2019 wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Enzi za uhai wake,Agnes amewahi pia kufanya kazi katika magazeti ya Uhuru,Mzalendo na Nipashe.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram,Zitto Kabwe ameandika:
Natoa pole sana kwa wana habari wote nchini kwa msiba wa dada Agnes Kabigi uliotokea Jana huko Kahama akiwa katika shughuli zake za kazi. Ni habari ya mstuko mkubwa hasa ukizingatia kuwa ni kifo cha ghafla sana. Mwenyezi Mungu awape subra wana familia wote kwa mtihani huu uliowapata. Ninamfahamu Agnes kama mwandishi dada mlezi. Wakati ninaanza harakati za vijana kupitia National Youth Forum ( NYF ) alikuwa mtu wa msaada mkubwa sana kwangu na kwa movement nzima chini ya kaka zetu Hebron Mwakagenda na Israel Ilunde. Agnes alikuwa mwanahabari mwandamizi aliyetekeleza wajibu wake kikamilifu. Mola amweke mahala pema peponi. Ameen
Social Plugin