Bodi ya lugha ya kusini mwa Afrika (PanSALB) jana imepongeza azimio la Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) la kutangaza kuwa itaitumia Kiswahili kama lugha rasmi ya nne ya mawasiliano.
Mwenyekiti wa bodi hiyo Bw. David Maahlamela amesema, mafanikio hayo muhimu ya kutambuliwa na kuongezwa kwa lugha asilia ya Afrika katika kanda hiyo ni juhudi kubwa kwa kuhakikisha maendeleo, matumizi na taaluma ya lugha za urithi katika eneo hilo.
Maahlamela amesema, kwa hatua hiyo, kwa sasa Kiswahili ndo kitakuwa Lugha pekee na ya kwanza ya Asili kutumika ndani ya bara la Afrika kati ya taifa moja la jingine ambayo ni wanachama wa SADC.
Amesema, Afrika ndo bara pekee ambalo watoto huanza kufundishwa shuleni kwa lugha za kigeni huku waafrika walio wengi wakipotoshwa kuwa Lugha za Kigeni kama Kingereza, Kifarasa, Kireno ndo Muhimu zaidi kwa taifa la Kiafrika kupiga hatua yoyote ya maendeleo
Social Plugin