Watu wanne wamepoteza maisha na wawili kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuyumba nje ya barabarani kabla ya kugonga miti na kuingia kwenye bonde wakiwa njiani kurejea Nairobi baada ya kuhudhuria mazishi Eneobunge la Kiharu.
Ajali hiyo imetokea Jumanne, Agosti 6,2019 katika eneo la Ithe Ruui kwenye Barabara ya Kenol-Murang’a nchini Kenya.
Inaelezwa kuwa watu hao sita walikuwa njiani kurejea Nairobi baada ya kuhudhuria mazishi Eneobunge la Kiharu, wakati dereva alipopoteza mwelekeo wa gari hilo na kuyumba nje ya barabarani kabla ya kugonga miti na kuingia kwenye bonde.
Kamanda wa Polisi Kaunti ya Murang’a Josphat Kinyua alisema wanne kati ya watu hao walifariki dunia mara baada ya ajali hiyo kutokea.
Kwa mujibu wa Citizen Digital, wawili walionusurika walipelekwa katika Hospitali ya Maragwa wakiwa na majeraha mabaya.
Ingawa chanzo cha ajali hiyo hakikujulikana mapema, wakazi katika eneo hilo walisema kwamba, eneo hilo linafahamika sana kwa ajali nyingi kaunti hiyo.
Miezi miwili iliyopita, naibu chifu wa Nginda aliripotiwa kuaga dunia kufuatia ajali ya barabarani eneo hilo.
Pia Waziri wa Maji wa Kaunti Water Paul Macharia, alihusika katika ajali ambayo ilimuua dereva wake kwenye barabara hiyo.
Social Plugin