AWESO CUP YAZINDULIWA KWA KISHINDO TARAFA YA MKWAJA WILAYA YA PANGANI, MBUNGE AWESO AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU SHIRIKI ASEMA MBWANA SAMATA,NGASA WANAWEZA KUPATIKANA KUPITIA LIGI HIYO

 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah katikati akimkabidhi vifaa vya michezo mmoja wa viongozi wa timu zinazoshiriki Ligi ya Aweso Cup Tarafa ya Mkwaja wilayani Pangani iliyoanzishwa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia anayeshuhudia lengo kuinua soka la wilaya hiyo
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah kushoto  akimkabidhi vifaa vya michezo mmoja wa viongozi wa timu zinazoshiriki Ligi ya Aweso Cup Tarafa ya Mkwaja wilayani Pangani iliyanzishwa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia anayeshuhudia lengo kuinua soka la wilaya hiyo
 Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso  kushoto akimkabidhi mpira mmoja wa viongozi wa timu zinazoshiriki Ligi ya Aweso Cup Tarafa ya Mkwaja mara baada ya kuizindua
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah katikati  akimkabidhi vifaa vya michezo mmoja wa viongozi wa timu zinazoshiriki Ligi ya Aweso Cup Tarafa ya Mkwaja wilayani Pangani iliyanzishwa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia anayeshuhudia lengo kuinua soka la wilaya hiyo
 Sehemu ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji kwa timu 10 zinazoshiriki Ligi hiyo Tarafa ya Mkwaja wilayani Pangani
 Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso  akizungumza wakati akizindua Ligi ya Aweso Cup Tarafa ya Mkwaja
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ligi hiyo
  Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akitoa nasaha kwa timu zinashiriki Ligi hiyo
  Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia akisalimiana na wananchi wa Tarafa ya Mkwaja wilayani Pangani wakati alipokwenda kuzindua Ligi ya Aweso Cup
 Wasanii wa Bongo Movie wakitoa burudani wakati wa uzinduzi huo
 Umati wa wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa Ligi hiyo
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa Ligi hiyo

MASHINDANO ya Ligi ya  Aweso Cup  Tarafa ya Mkwaja wilayani Pangani Mkoani Tanga yamezinduliwa rasmi huku yakishirikisha timu 10 ambao zimekabidhiwa vifaa vya michezo tayari kwa ajili ya ushiriki wao 

Uzinduzi wa Ligi hiyo umefanywa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji ambaye amekuwa akidhamini mashindano hayo kila mwaka lengo kubwa likiwa kuibua vipaji vya wachezaji wachanga wilayani humo. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Aweso alisema kwamba michezo ni ajira ambayo inaweza kuwainua vijana na kuweza kuwakwamua kimaendeleo hivyo wanapaswa kucheza kwa nidhamu na kuonyesha jitihada. 

“Kila siku nimekuwa nikisema kwamba kikubwa zaidi ni kutaka kuibua vipaji vya wachezaji lakini tokea tumeanzisha ligi hii tumepata mafanikio makubwa ikiwemo kuoandisha timu nne kucheza Ligi ya mkoa wa Tanga lakini pia ninaimani kwamba siku zijazo tutapata timu ya Ligi Daraja la kwanza na Ligi kuu “Alisema 

Aidha pia aliwataka vijana wa Mkaramo na Mkwaja ambao wamepata fursa ya kushiriki kwenye Ligi hiyo kuhakikisha wanaonyesha vipaji vyao ikiwemo kutanguliza nidhamu wawapo michezo ili kuweza kupata mafanikio. 

“Ndugu zangu wanamichezo wenzangu mmepata fursa hii onyesheni vipaji kwani baadae tutaunda timu ya Tarafa ambayo itakuwa ikicheza na timu nyengine kwa lengo la kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji waweze kuonekana”Alisema 

Aidha alisema pia kwamba ni matumaini yake kwamba kupitia Ligi hiyo vipaji vya wachezaji vinaweza kuibuliwa na hatimaye kuweza kupatikana wachezaji wenye uwezo kama akina Mbwana Samata na Mrisho Ngasa 

“Lakini pia niwapongeza kamati ya ulinzi na usalama kwa kuwezesha ulinzi kuwepo kwenye mchezo nipongeza kamati ya Ligi tarafa ya Mkwaja na chama cha mpira wilaya kwa kazi kubwa na nzuri mnazofanya kuwaunganisha vijana kwenye michezo”Alisema. 

“Pia leo hii tumebahatika kuwa na Wasanii wa Bongo Movie hapa ambao ni wazawa wa Pangani Kupa, Truda na Mtanga wasanii wamefika hapa kuwaunganisha na wasanii wengine muweza kutoka kupitia medani hiyo”Alisema 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah alisema kinachofanywa na Mbunge huyo katika michezo ni jambo nzuri kutokana na kwamba ni mahali ambapo vijana wanaweza kuitumia kupata ajira na kuweza kujikwamua kiuchumi. 

“Ndugu zangu niwaambie kwamba michezo inaimarisha undugu, kujenga afya lakini pia ni ajira nzuri iwapo mtaizingatia na kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu “Alisema 

Kwenye Ligi hiyo mshindi wa kwanza atapata Ng’ombe, mshindi wa pili Jezi na wa tatu atapata mbuzi  ambayo itashirikisha timu za soka Mkalamo Stars,Sange FC,Buyuni,Mikocheni FC,Shirikishoni,Mkwaja Stars,Boza FC,Mbulizaga FC,Tongani Sekondari na Mtakuja

huku akitoa onyo kwa yeyote atakayotaka kushiriki kwa ajili ya kuleta fujo atashughulikiwa kwani hawatakubali kuona ligi inaharibika kwa ajili ya watu wachache. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post