Waandishi wa habari wanaoandika habari kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) inayohusisha Runinga za Mtandaoni 'Online Tv' na Blogu 'Blogs' wamejengewa uwezo kuhusu Kanuni za Maadili (Ethical Reportage ‘Code Of Ethics’) ili waweze kuandika kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari/taarifa zinazohusu ukiukwaji wa haki za binadamu, utawala bora na demokrasia.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika leo Alhamisi Agosti 22, 2019 na Agosti 23,2019 jijini Dodoma ni sehemu ya utekelezaji utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) unaoratibiwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia ya Klabu Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House na PACT.
Mwezeshaji wa Mafunzo ya Kanuni na maadili ya uandishi wa habari, Allan Lawa akitoa mada kuhusu maadili ya uandishi wa habari na kuwasisitiza waandishi wa habari mtandaoni kuandika habari bila uoga kwa kuzingatia ukweli na uweledi kwa kuzingatia misingi ya uandishi wa habari. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mwezeshaji wa Mafunzo ya Kanuni na maadili ya uandishi wa habari, Allan Lawa akitoa mada kuhusu maadili ya uandishi wa habari
Social Plugin