KAIMU katibu wa Umoja wa Wanawake(UWT) wilaya ya Geita Angela Simwanza amefanya ziara na kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Geita kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
Ujumbe huo umetembelea miradi mbalimbali katika kata ya kata ya Nyarwanzaja ikiwemo ujenzi wa ghorofa katika shule ya sekondari ya Nyarwanzaja.
Akizungumka katika ziara hiyo katibu Angela amemshukuru Rais dkt John Magufuli kwa jitihada anazozifanya za utekelezaji wa ilani.
"Rais wetu anafanya kazi kubwa sana ya kutuletea maendeleo, anatekeleza Ilani ya chama chetu na ametoa miradi ya CSR hivyo tuna kila sababu ya kueleza mafanikio haya ili watu wajue, "alisema katibu Angela.
Amewashukuru wabunge na madiwani kwa usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa.