Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)anayeshughulikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akizungumza na viongozi akiwataka wasaidie kuwahamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya ya jamii ya CHF iliyoboreshwa alipotembelea Zahanati ya kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino mkoani Dodoma kushuhudia utekelezaji wa kuandikisha Kaya katika mfumo huo.
Muuguzi wa Zahanati ya kijiji cha Chiboli ,Shija Makeja,akielezea jinsi wanavyoshirikiana na uongozi uliopo katika kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya ya jamii ya CHF iliyoboreshwa kushoto ni katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)anayeshughulikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akimsikiliza.
Meneja mradi wa HPSS Tuimarishe afya, Ally Kebby Abdallah,akizungumzia Azma ya Serikali ni kutengeneza mfumo wa bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa ni kuona mwananchi anatambuliwa lakini pesa anayochangia irudi kwenye kituo.
Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)anayeshughulikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akiangalia kibao kinachoonesha ratiba ya kazi katika Zahanati ya kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino mkoani Dodoma alipotembelea kushuhudia utekelezaji wa kuandikisha Kaya katika mfumo wa bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa.
Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)anayeshughulikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akiwahamasisha wananchi wa kijiji cha Chiboli wajiunge na bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa ili wafurahie huduma bora alipotembelea Zahanati ya kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino mkoani Dodoma kushuhudia utekelezaji wa kuandikisha Kaya katika mfumo wa bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa.
Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)anayeshughulikia Afya Dk.Doroth Gwajima,mkazi wa kijiji cha Chiboli anayetumia bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa jinsi inavyookoa maisha ya familia yake pindi anapopata na tatizo
***
Serikali imewataka viongozi wa serikali za Mitaa a vijiji nchini kusaidia kuhamasisha wanachi kujiunga na bima ya afya ya jamii ya CHF iliyoboreshwa ili waondokane na adha pindi wanapokuwa hawana fedha za mkononi kulipia matibabu.
Haya yamebainishwa na katibu mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)anayeshughulikia Afya Dk.Doroth Gwajima alipotembelea Zahanati ya kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino mkoani Dodoma kushuhudia utekelezaji wa kuandikisha Kaya katika mfumo huo.
Amesema suala la kuhamasisha wanachi kujiunga na bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa siyo jukumu la wataalam wa afya peke yao kwani wanaotakiwa kulisimamia ni viongozi wa vijiji ambao ndiyo waliokaribu na watu.
"Hili suala la watu kujiunga na bima hii ya afya ya jamii ya CHF iliyoboreshwa ni suala la kushirikishana hawa viongozi wa vijiji kama mwenyekiti wa kijiji na afisa mtendaji wa kijiji ndiyo wenye watu na wenye mikutano ya hadhara ambayo ajenda hii wataifikisha kwa njia rahisi"amesema Dk. Gwajima.
Pia Dk. Gwajima amesema kuwa kama viongozi wa serikali za vijiji watakuwa na ushirikiano na wataalamu wa vituo vya afya nchini wataweza kuibeba ajenga hiyo kwa kuifikisha kwa wanachi na kuweza kuziandikisha kaya zote nchini katika mfumo huo wa CHF iliyoboreshwa.
Kwa upande wake Muuguzi wa Zahanati hiyo Shija Makeja,amesema kuwa kupata mafanikio ya kuwa na idadi kubwa ya wanachama wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kumetoka na kushirikiana kwa karibu na viongozi wa serikali ya kijiji.
Amesema kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya watu wanaotumia CHF iliyoboreshwa wameweza kupata fedha za kujiendesha na kuondokana na changamoto za ukosefu wa madawa ambao awali ulikuwa kikwazo.
Nae Meneja mradi wa HPSS Tuimarishe afya, Ally Kebby, amesema kuwa azma ya serikali ni kutengeneza mfumo wa bima ambao mwanachi atatambuliwa na pesa anayochangia itarudi kwenye kituo.
Mradi wa HPSS Tuimarishe afya unafadhiriwa na shirika la maendeleo na ushirikiano la Uswisi kwa kushirikana na serikali ya Tanzania ambao umechangia katika kuunda mfumo wa kutendea kazi wa IMIS na kutoa mafunzo kwa waandikishaji waratibu na wasimazi wa CHF iliyoboreshwa nchini.
Social Plugin